Waziri wa Afya ni bora ungeanza na mchakato wa Bima ya Afya kwa kila Mtanzania kuliko kutoa agizo kama hili

Uwezo wako wa kudadavua mambo ni very low, huwezi kuoanisha mfano wa kumuona mbunge na ishu ya kumuona daktari.

Hapa jukwaani kuna mtu amesema waziri haiwezi hii wizara?

Hoja ni kutaka kuhoji uwezo wa mgonjwa kulipia gharama wakati anahitaji matibabu.

Suala la cost sharing linahitaji ufafanuzi na shule? Maana miaka ya tisini serikali ilianzisha hii kitu,hasa baada ya kuona haina pesa za kutosha kugharamia huduma za afya. Unaposema watu tujustify kwa nini kuna pesa ya kumuona Dk,wewe una akili timamu?
 
Kama elfu 10 huna halafu na kujieleza kwa ndugu,majirani pia hujui hilo ni tatizo lingine.
Au wewe kwenye ukoo wenu umezaliwa peke yako?
Hayo ni mengineyo,la sivyo tusingekuwa tunasikia watu wanazuiwa kutoka Hospital au maiti zinazuiwa.
 
Hiyo ni kweli mkuu ila shida gharama zenyewe hazina uhalisia.
Kumdai mfiwa milioni 10 kama gharama ya mortuary tena kwenye hospitali ya umma haina uhalisia
Kwenye magharama hapo ndiyo waangalie na kurekebisha lakini tukisema sijui watu wasilipie gharama ya mwili hiyo ni fiksi tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni mbumbu wa kufa,hizo modules zinahusika vipi na watanzania kushindwa kulipia matibabu kisha kufariki?

Toa ujinga wako wa kukariri unashindwa kujadili suala simple ambalo hata mtoto wa la kwanza analielewa.
 
Kwenye magharama hapo ndiyo waangalie na kurekebisha lakini tukisema sijui watu wasilipie gharama ya mwili hiyo ni fiksi tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Hivi kwani gharama ya kuhifadhi mwili kwenye hospital za umma ni sh ngapi? Wewe kwa nini usishauri wenye pesa wawe wanaenda private hospital,alafu za umma iwe bure kabisa? Maaana sasa pato la taifa linaenda kuongezeka mpaka tril 2.
 
Inasikitisha sana...
Yale yote uliyoyasikia kipindi cha karibia na uchaguzi yasikuumize kichwa, zile zilikua ni siasa...

Hii sasa ndiyo hali halisi... Na bado...




Cc: mahondaw
 
Sekta ya afya ina changamoto sana....hiyo bima sio jambo dogo.
Ila huyu mama apunguze mdomo..asikilize ushauri itamsaidia sana.
 
Ila kusema tu ule ukweli hii wizara safari hii imepata waropokaji kweli kweli halafu wanajikuta 'majiwe kweri kweri'.

Anakopita waziri kila sehemu matamko tu na 'skafu' yake yenye bendera ya Tanzania, hivyo hivyo anakopita Naibu wake yeye ndio anasimamisha watu kazi utafikiri ndio suluhu vile.

Wakiwa pamoja sasa utafikiri ni kikundi flani cha comedian, Waziri anaongea jambo halafu anamuangalia Naibu wake na kumuuliza kama kweli, then Naibu anatikisa kichwa na kusema eeeh kweli [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Angalau angewekwa Faustine huyo mama nakuambia hatoboi mwaka hapo
Bro
Awamu hii wakurupukaji wanapendwa na rais keeli kweli.
Hasa wapenda kamera na watoa matamko lukuki
 
Kwa mfumo ulipo sasa Tanzania haina uwezo wa kutoa bima bure kwa kila mtanzania....hiyo kauli ilikuwa ya kiwahadaa watanzania kwenye uchaguzi...Elimu yetu yenyewe ni tia maji tia maji iweje Bima Bure?
 
Hii ishu ya bima ya afya ni umiza kichwa kwa kweli. Hata wanaotumia hiyo hawapati huduma za muhimu......
 
Huu upuuzi unaoweka kama randama unamsaidia nini mtanzania asiyeweza kugharamia gharama za matibabu?
 
Kabla kabisa waziri wa Fedha angekuja na mkakati wa kodi kwa kila kichwa.. then wa afya atoe tiba kwa kila mtu bure na wa elimu atoe elimu bure na wakazi atoe ajira za kutosha na ikishindikana Watu wapewe hela tuu.. hata kama kazi hakuna.
 
Bima ya afya ni muhimu sana kwa kila mwananchi lakini pia gharama za matibabu ni kubwa sana duniani pote.

Kuweza kufikia malengo ya kuwa na bima ya afya kwa kila mwananchi sio swala la kulala kuamka na kuamua tuu. Tukumbuke hii sio gharama ya Mara moja kwa mwaka ila ni gharama ya kila siku na gharama endelevu.

Kabla ya kuingia kwenye ujumla wa bima ya afya serikali kupitia sekta husika ifanye uchambuzi yakinifu kupata makundi ambayo yanaweza kuanza kuchangia huduma hii, makundi ambayo yanalazimika kupata huduma bure, na pia uboreshwaji uwekezaji na uzalishaji mali viende hatua kwa hatua na uchangiaji wa huduma ya afya kwa wadau wake

Shirika lenye mamlaka ya afya ya taifa NHIF nalo watafute njia ya kupunguza gharama za uendeshaji kwa kuondoa gharama zisizo za lazima na kufocus kwenye kutoa huduma kwa wateja wake tuu na huduma wanazotoa ziwe kwa gharama nafuu kwa wateja wao vikiwemo vituo vya afya na mahospitali
 
Kwangu mimi huyu wa Waziri wa afya ndiye waziri wa hovyo zaidi.
Ni mpenda sifa na mkurupukaji.
Anafanya vitu kwa sifa na hana weledi wowote.
Wewe una akili na umeona vema, anapenda sana sifa hata za kipumbavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…