Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa aagiza wanaotuhumiwa kusababisha migogoro ya ardhi Mbondole (Ilala) wakamatwe

Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa aagiza wanaotuhumiwa kusababisha migogoro ya ardhi Mbondole (Ilala) wakamatwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ameagiza kukamatwa kwa Watu kadha ambao wanatuhumiwa na Wananchi kwa kusababisha migogoro ya ardhi na kuuza maeneo kinyume na taratibu kwa wakazi wa Mbondole, Kata ya Msongola Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Waziri Silaa ametoa maagizo ya kukamatwa watu hao wakati alipofanya ziara katika eneo hilo linalomilikiwa na Taasisi ya Green foundation tangu Mwaka 2017.

Kwa mujibu wa Waziri Silaa eneo hilo limekuwa likizuwa taharuki kwa wananchi ambao wameuziwa viwanja kinyemela na watu hao waliovamia mali ya Green foundation ambao ndio wenye nyaraka za umiliki wa eneo hilo.
 
Back
Top Bottom