Nimesoma maelezo yako nakubaliana nayo,isipokuwa nakusahihisha kiswahili fasaha,nano upungufu halina wingi yakiwa mengi ni upungufu na likiwa moja ni upungufuMh. Pamoja na kwamba kuna usemi: don't judge book by its cover, uhalisia ni kwamba wakati mwingine umbile la nje la kitabu linaakisi yaliyo ndani. Kwa binadamu mavazi yako yanaakisi hadhi yako, kwa vitu kama magari, simu, nyumba nk. Vinaakisi hali ya ndani ya vitu hivyo. Nimeshtushwa sana kuona fomu ya kujiunga ya sekondari ya wasichana ya Beatrice Shelukindo ina mapungufu ya kutisha.
Fomu hiyo inapatikana katika mtandao wa wizara kama kiambatanisho kwa waliochaguliwa kujiunga na shule hiyo: Uchaguzi wa Kidato cha Kwanza, 2026
Mapungufu yaliyo kwenye fomu hiyo huenda yakaashiria, udhaifu wa weledi wa kiongozi wa shule hiyo, au ushirikishwaji mdogo wa watendaji, au udhaifu wa wasimamizi, au kutojali, au uduni wa taaluma ya elimu na ualimu au vyote na zaidi kwa pamoja.
Naomba uipitie fomu hiyo na ikikupendeza ufananishe na fomu ya Sekondari ya Kilindi Girls
Kwa mazingira ya Kitanzania yaweza tu kuwa hujuma za ndani kisa yupo anayeitamani ukuu wa shule ama yanayofanana na hayo.Na bahati mbaya inaweza kuwa ndiye mpandisha mada,japo nia ya sii kumshutumu ama kumdhihaki ila nazungumzia mazingira yetu ya Kitanzania ya kila siku,makazini na zinapopatikana riski.Mh. Pamoja na kwamba kuna usemi: don't judge book by its cover, uhalisia ni kwamba wakati mwingine umbile la nje la kitabu linaakisi yaliyo ndani. Kwa binadamu mavazi yako yanaakisi hadhi yako, kwa vitu kama magari, simu, nyumba nk. Umbo la nje linaakisi hali ya ubora iliyop ndani ya vitu hivyo.
Nimeshtushwa sana kuona fomu ya kujiunga ya sekondari ya wasichana ya Beatrice Shelukindo ina mapungufu ya kutisha.
Fomu hiyo inapatikana katika mtandao wa wizara kama kiambatanisho kwa waliochaguliwa kujiunga na shule hiyo: Uchaguzi wa Kidato cha Kwanza, 2026
Mapungufu yaliyo kwenye fomu hiyo huenda yakaashiria, udhaifu wa weledi wa kiongozi wa shule hiyo, au ushirikishwaji mdogo wa watendaji, au udhaifu wa wasimamizi, au kutojali, au uduni wa taaluma ya elimu na ualimu au vyote na zaidi kwa pamoja.
Naomba uipitie fomu hiyo nimeiambatanisha hapa chini.