DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mnaona mambo rahis eeeh hio elimu yakukariri tu mashule hayana vitabu nachaki leo uanzishe kusoma kwaprojector, demonstration, laboratory.... Nchi kama inashindwa kusambaza maji mkoa wamwanza wenye ziwa utaweza hayo
Mambo ni rahisi tu Wala hakuna ugumu wowote, tatizo ni mind za watu wanaofanya maamuzi, hii nchi siyo masikini ila watu ndo masikini na umasikini unadumaza akili, hivyo wafanya maamuzi wanatakiwa kufanya maamuzi ya kuvusha watu wengi na siyo kuacha watu wachache wajifaidishe kunyonya kile kidogo wenzao waliochokitafuta kwa kisingizio Cha kuwafundisha zaidi na zaidi eti ndo watafaulu haya masomo ya kukalili wakati wao wanachohitaji ni pesa za wazazi wao, tabia za watu wote kwenye nchi zinatakiwa zipimwe mara kwa mara kwa kutumia Sheria na hasa watu wazima wanapojikusanya sehemu Moja huwa wanafundishana ujinga au werevu, Sasa hawa walimu na wenye shule wamefundishana ujinga wa kutapeli wenzao kupitia watoto wao, ni kwamba wanafanya watoto wasio na kosa kuwa mateka wao wa kujifanya kuwa overdose masomo ili wao watapeli pesa kwa wazazi wao, hapo waliowapa huo mwanya niwatunga Sheria za watoto wanaosoma.
 
  • Hata shule za serikali wanabaki ndg! Huu ujinga ulianzia shule binafsi, ukaachwa na sasa umefika mpaka shule za serikali.
  • Ni moja ya mambo yanayoongeza gharama za maisha.
  • Watu wanaotetea haki za watoto hawasikiki ktk hili.
  • Watoto hawajui kazi ndogondogo kama kupika maandazi kibiashara, n.k Kwa kuwa muda wote - usiku na mchana - 'WANATAFUTA THAMANI YA X'; mbaya zaidi haiwasaidii kupambana na maisha.
  • Waziri wa Elimu atakwa via ni jukumu la TAMISEMI; usishangae TAMISEMI wakakwambia ni hiari kutoa ama kutotoa. Mambo ya kitaifa yanafanywa kiholela.
  • Wabunge wapo tayari hata kurusha ngumi kutetea huu utaratibu kwa kuwa wanamiliki shule au watetea shule za washkaji zao.
  • Huko duniani msisitizo upo kwenye ubunifu, huku kipaumbele ni kufaulu

Naunga mkono hoja 💯💯.
Kwa sasa ubunifu kwa watoto umepotea kabisa!
Watoto wakibaki nyumbani wanafanya hizo kazi? Acheni unafki
Watoto wakiwa nyumbani kazi ni kuangalia TV,kushinda beach,kucheza game na upuuzi mwingine
Acheni unafki
 
Mbona umecomment kwa kutoheshimu mawazo ya mwenzako halafu kama unamjibu kwa dharau na chuki debe nzima. Punguza hasira na jazba huu ni mjadala wa kijamii sio mjadala wa mtu binafsi.
Unanifundisha kujibu,we si umjibu unavyoona inafaa, au ndiyo nyie mnasomeshwa ulaya kwa hela ya watanzania,mnataka watoto wetu waendelee kuwa watumwa wenu?
 
Acha uzoba Kwan Max ni wazir wa elim ?
Una umri gani hapa?...haya yanayoongelewa hapa ni makubwa kuliko uwezo wako wa akili na umri. Umehitimu darasa la saba miaka minne iliyopita na kufeli mtihani wa kidato cha pili hata kuandika tu huwezi je utaweza kujadili maswala haya mazito ya kitaaluma?

Hatuandiki hapa kukufurahisha ni kwa ajili ya kuboresha elimu yetu na watu kama wewe ambao ni zao halisi la elimu yetu na mfano dhahiri wa kijana umri wako uliyeishia kidato cha pili hata kuandika sentensi sahihi huwezi!
 
Acheni watoto wasome, wakifeli mtaanza tena oo walimu hawafundishi, wakijitolea hata muda wa likizo oooh watoto warudi kumpumzika, wazazi wengine ni tatizo aseee🤔🚮🚮
 
Hili swala la elimu na mitaala limekuwa kama kichwa cha mwendawazimu. Kila mtu anajiamulia atakavyo.

Kuna baadhi ya shule kama Diamond na Olympio watoto wanaenda shule mpaka j2.
Safi kabisa, ila mtoto wako akipata wastani wa A" utakuja hapa kuwafungulia uzi hao diamond kwamba ni shule bora
 
Kiukweli ata mwanangu, jumamosi anaenda, na amenidokeza awatafunga shule.
 
Nenda shuleni waambie mwanangu naondoka naye akapumzike,bila shaka watakusikiliza.
 
Una umri gani hapa?...haya yanayoongelewa hapa ni makubwa kuliko uwezo wako wa akili na umri. Umehitimu darasa la saba miaka minne iliyopita na kufeli mtihani wa kidato cha pili hata kuandika tu huwezi je utaweza kujadili maswala haya mazito ya kitaaluma?

Hatuandiki hapa kukufurahisha ni kwa ajili ya kuboresha elimu yetu na watu kama wewe ambao ni zao halisi la elimu yetu na mfano dhahiri wa kijana umri wako uliyeishia kidato cha pili hata kuandika sentensi sahihi huwezi!
[emoji28][emoji28]
 
Safi kabisa, ila mtoto wako akipata wastani wa A" utakuja hapa kuwafungulia uzi hao diamond kwamba ni shule bora
Nina hakika wewe ni mwalimu wa Diamond na umehisi kama maslahi yako yanahatarishwa,

Ikiwa mtu mzima tu anapumzika sembuse mtoto. Sisi tulisoma elimu hiyo hiyo na likizo tulikaa majumbani, hatukwenda shule Jumamosi na Jumapili lakini tulimaliza na leo tuna watoto. Nini cha mno kilichobadilika kwa sasa?
 
Mheshimiwa Waziri,

Kumekuwa na mtindo wa wamiliki wa shule kuamua tu kwa utashi wao kubakiza watoto shuleni(madarasa ya mitihani) kwa kigezo kwamba wapate muda wa kumalizia mitaala tena bila kushirikisha wazazi huku wakiwa tayari wamepanga na gharama zao.

Hivi walimu wanashindwa vipi kumaliza mtaala kwenye muda uliopangwa?Kibaya zaidi wamekuwa wakiongeza gharama za ziada za Tuition fee na transport hasa kwa shule binafsi.

Sasa kama lengo la walimu ni kumaliza mtaala hili si jukumu lao,kwanini gharama zirudi kwa mzazi?

Je ni sahihi mtoto kusoma bila kupumzika?Kuna watoto wanasoma mbali na wazazi wanahitaji kuonana na wazazi wao ambao hawajawaona kwa muda mrefu,sasa kumshikilia mtoto shuleni muda mrefu kisaikolojia imekaaje?

Mimi binafsi naona shule zimeamua kubuni tu mradi wa kujipatia kipato kwa kigezo cha kumaliza mitaala.

Tayari kuna shule zimeshatoa taarifa kwamba darasa la nne hawatafunga shule ili waendelee kufundishwa,Je mmeruhusu?

Tunaomba hili suala lizuiliwe kisheria na sio kwa matamko ya kila mara maana nakumbuka mwaka Jana ulitoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleni ila naona linajirudia tena.

Pia soma: Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo

Ahsante.
Mkuu ahsante kwa Uzi wako,naona waziri wa elimu kapigilia msumari ,watoto waende likizo
 
Mkuu ahsante kwa Uzi wako,naona waziri wa elimu kapigilia msumari ,watoto waende likizo
Mkuu asante,nilikuwa safarini leo kumchukua mtoto nafika nyumbani ndio napewa taarifa kwamba waziri kazuia,kwa pamoja tumefanikiwa katika hili.

Pongezi nyingi ziende kwa uongozi wa JF
Maxence Melo and Team!
 
Back
Top Bottom