DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ametekeleza kwa tamko... Haya matamko sawa tu na yaliyo kwenye kanga ambazo wanawake wanajifunga kiunoni na maandishi kusomeka yakiwa yamejipanga sawasawa kati ya mtikisiko wa zegembe!! Wanafunzi wapo shuleni kama kawaida !!!
Kuna barua ya wizara nimeattach hapo juu, na kwenye uzi wangu nilisema katazo liwekwe kisheria na adhabu zake kwa mkiukaji,hata hivyo shule nyingi za binafsi watoto wamerudishwa,hizo zingine sijui labda ufuatiliaji hakuna.
 
Tanzania ni moja kati ya nchi zanazo shangaza duniani!! Fikiria mtu anaamka TU anasema shule hazitafungwa ( Yani tafsiri yake hakuna mwanafunzi kuwa na likizo) Halafu watu wanakaa kimya!!
Utadhani hakuna mamlaka husika,watu wanajiamulia tu
 
Sasa imeshaingilia watoto wanahaki ya kupumzika!! Kama ulifikiri utapiga pesa pole ndugu yangu!! Tafuta kazi nyingine!!
[emoji2][emoji2][emoji2],Hao ni wale ambao maslahi yao yameguswa
 
Mheshimiwa Waziri,

Kumekuwa na mtindo wa wamiliki wa shule kuamua tu kwa utashi wao kubakiza watoto shuleni(madarasa ya mitihani) kwa kigezo kwamba wapate muda wa kumalizia mitaala tena bila kushirikisha wazazi huku wakiwa tayari wamepanga na gharama zao.

Hivi walimu wanashindwa vipi kumaliza mtaala kwenye muda uliopangwa?Kibaya zaidi wamekuwa wakiongeza gharama za ziada za Tuition fee na transport hasa kwa shule binafsi.

Sasa kama lengo la walimu ni kumaliza mtaala hili si jukumu lao,kwanini gharama zirudi kwa mzazi?

Je ni sahihi mtoto kusoma bila kupumzika?Kuna watoto wanasoma mbali na wazazi wanahitaji kuonana na wazazi wao ambao hawajawaona kwa muda mrefu,sasa kumshikilia mtoto shuleni muda mrefu kisaikolojia imekaaje?

Mimi binafsi naona shule zimeamua kubuni tu mradi wa kujipatia kipato kwa kigezo cha kumaliza mitaala.

Tayari kuna shule zimeshatoa taarifa kwamba darasa la nne hawatafunga shule ili waendelee kufundishwa,Je mmeruhusu?

Tunaomba hili suala lizuiliwe kisheria na sio kwa matamko ya kila mara maana nakumbuka mwaka Jana ulitoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleni ila naona linajirudia tena.

Pia soma: Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo

UPDATE:

Wizara imeitikia wito wa wadau, soma Serikali: Wanafunzi wasizuiwe kwenda likizo
Kuna Mambo kadhaa ya kurekebisha kwenye Mitaala na Miongozo ya Elimu Tanzania…

Ni Mwendo wa kukariri tu. Hakuna Skills
 
Kabisa mkuu... Hii hali sio ya kuilea. Tunawaharibia watoto future... Wanakosa hata muda wa ku synthesise kile wanachondishwa, wanameza tu
Sipendi utaratibu wa kubaki shuleni Mimi ..nauchukia walimu Wa Dar na private ndo Sanaa...
Dar walimu Wa kayumba primary ni Kwa sababu ya 500,500 za watoto
 
Sipendi utaratibu wa kubaki shuleni Mimi ..nauchukia walimu Wa Dar na private ndo Sanaa...
Dar walimu Wa kayumba primary ni Kwa sababu ya 500,500 za watoto
Sio mzuri kabisa. Na hapo bado wanakuwa wanaamshwa saa 10 alfajiri na kulala saa 5... Cheiii sijui wanajazwa nini ambacho wengine hatukusoma
 
Mkoloni amejua wapi pakutukamata, vichwa vya watoto vimegeuzwa hard disk ya kumeza tu baada ya hapo hamna kitu, elimu ambayo hakuna sehemu tuna apply.
Nayakubali sana mataifa ya Asia mfano China na Korea ya Kaskazini hawana elimu ya mkoloni
 
Na tunameza kwa kweli…hadi uchafu
 
Mkoloni amejua wapi pakutukamata, vichwa vya watoto vimegeuzwa hard disk ya kumeza tu baada ya hapo hamna kitu, elimu ambayo hakuna sehemu tuna apply.
Nayakubali sana mataifa ya Asia mfano China na Korea ya Kaskazini hawana elimu ya mkoloni
Wanamezeshwa vitu ili waje kujibia mtihani
 
Sio mzuri kabisa. Na hapo bado wanakuwa wanaamshwa saa 10 alfajiri na kulala saa 5... Cheiii sijui wanajazwa nini ambacho wengine hatukusoma
Miradi ya upigaji tu tu Kuna likizo watoto wapumzike
 
Back
Top Bottom