DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kati ya deal za hovyo kufanya ni zile zinazohusu watoto wetu ambao tunawategemea waje watuongoze Tanzania. Tushirikiane kusema hapana kwenye deals hizi za kijinga mpaka viongozi washtuke
Ni kweli hizi deals zinaua kizazi cha kesho,tucheze na hela ila sio watoto wetu,hii tabia lazima ikomeshwe
 
walimu wengi wapo wapo kama mayatima,hawana cha kufanya,kuna jamaa hapa shuleni kwangu alitaka kunitwanga ngumi nilipokataa wazo la watoto kubaki wakati wa likizo,cha ajabu malipo kwa kila mtoto ni sh 1000 na watoto wao 400, walimu waliokubaliana na huo mpango wako saba,1000x400= 400,000÷7= 57,000 kwa muda wa wiki tatu,

Walimu tunakwama sana.
 
Kunasiku niliutoa huu Uzi nikashambuliwa mno na watu
Mkuu usijali kushambuliwa,humu kuna wajinga wapo wanaishi magetoni wala hawafikirii kuoa wala kuolewa,wao wakiamka na kula na kulala inatosha ndio maisha

Wengine kataa ndoa,wengine ma- wimpy kids sasa lini atawaza kuhusu hatma ya watoto?
 
Wazazi siyo wajinga kwa issue kama hii, kinachofanya wazazi wanakaa kimya kwa issue kama hii ya kuiwaibia pesa au kutapeliwa pesa na shule kwa kisingizio Cha darasa la mtihani nikulinda utu wa watoto wao, maana wewe mwenye shule bila aibu unaleta hoja kama hiyo ya kuwatumia watoto kujipatia pesa za kinyonyaji na naita za kinyonyaji kwasababu angekuwa yeye au hao walimu wanaoandaa hizi mbinu za kunyonya asifurahi kwenye moyo wake na hapo mzazi mpingaji sana unakuta mtoto wake anafelishwa na kwa muda huo wa mitihani wanajua mzazi hawezi kuhamisha mtoto ndo maana wanakaa kimya ili baada ya mitihani wachukue hatua.

Sasa kwa vile jamii ya watoto inaangamia kwa maumivu ndo wazazi Sasa wachukue hatua kumjulisha waziri wa elimu na waziri wa ustawi wa jamii washughulikie kisheria na hata uongozi wa juu kabisa uwajibike kuwasaidia watoto kwa kuwatengenezea Sheria ya kuwalinda na masomo ya shule pamoja na likizo kama ilivyo kwa wafanyakazi zipo Sheria za kuwalinda ila watoto wadogo wa shule hawana Sheria za kuwalinda zinazoweza kutumiwa na wazazi kuwashitaki hao walimu na shule za wakola, nasema niwakola kwasababu huwa wanafanya makusudi kutofundisha kwa wakati ili waje wanyanyase watoto kwa hiyo tiatia maji au overdose ya masomo mpaka watoto wanaathirika.

Kingine hii kitu inahitaji watu au wazazi wasimame kweli maana hao wanaotakiwa kufanya maamuzi magumu ili kuwanusuru watoto na overdose ya masomo wengine ndo wenye shule hizo, wengine walimu wanaojipatia hizo pesa, wengine wanahongwa kupinga maamuzi mazuri, mfano pale wizara ilipoondoa kuonyesha shule Bora Bali ikataka waonyeshwe wanafunzi Bora hapo tumeona kelele nyingi sana, shule zikilazimisha zionyoshwe Bora badala ya kuonyesha wanafunzi Bora, Sasa hapo watoto wa shule wanazidi kuumia kwa kushindwa kutengenezewa Sheria za kulinda, waziri anasema tu shule zifungwe bila kusema asiyefunga shule yake basi yeye ndo afungwe ili asiumize watoto, alafu ukakuta walimu wao wanajipa likizo kwa kupokezana ila watoto ndo wanakuwa overdose ya masomo, ya kuamuka usiku, mabegi mazito yaani nikuwa overdose watoto mpaka wengine wakiuguwa kidogo tu wanafariki maana mwili Hauna afya.
 
Ni kweli sheria inatakiwa iseme,kama ambavyo shule zinafungwa tarehe fulani basi na shule zisizofungwa pia kuwe na adhabu,hii ndio itakuwa namna nzuri ya kudhibiti hili
 
Pengine wanataka watoto wapate muda mwingi zaidi wa kufundishwa mapenzi ya..
 
kwa kweli mimi kama mwalimu nafuata siku za kufundisha zilizopangwa na serikali, hiyo mipango inayopangwa na mkuu wangu wa shule kwa kushirikiana na baadhi ya walimu huwa sifuati utaratibu huo nina mambo yangu muhimu ya kufanya wakati wa likizo za wanafunzi. Kama hoja ni kukimbiza mada huwa najiamini kumaliza mada zote mapema tu na nabakiwa na muda wa marudio kwa mada ngumu ambazo hazikueleka vema kwa wanafunzi wote. Nibaki shuleni wakati wa likizo mwalimu mkuu atanimegea mshahara wake? Afundishe yeye kama ana muda huo mi naenda kwenye mishe zingine. Wakaguzi wa elimu wakija kunikagua wanakuta niko fiti
 
Walimu wa siku hizi kichwani hamnazo, wanafululiza kuchosha wanafunzi wakati misingi ya elimu haitaki upuuzi huo. Mwanafunzi lazima apumzike ili aweze kupokea maarifa mapya katika muhula unaofuata. Kanuni za ufundishaji zinataka hivyo. Ukimfululizia mwanafunzi kumfundisha hataelewa unafundisha nini utamvuruga katika kutafakari na kufanya maamuzi katika kujifunza
 
[emoji2][emoji2]
 
Hii nchi ukichukulia serious utakufa siku si zako. Rais mwenyewe ndo huyo
 
Kupumzika muhimu sana tu
 
Kawaida ndio mikakati hiyoo,Unafikirii kufaulisha watoto ni mchezo,inahitaji juhudi.Mtu unalalamika ukute mtoto wako mwenyewe tia majimajii kwenye taaluma......so liachwe liwape zero
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…