DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kama ni kubadilisha mitaala ibadilishwe tu,ila kuwabana watoto namna hii haifai na wala sio afya kabisa,mbaya zaidi inazalisha gharama zaidi kwa mzazi
 
Sambamba na hilo Max, liende pia hili la upigaji wa kambi za kimasomo katika shule ambazo si za bweni!
Pamoja upigaji kambi, na hili la michango iliyozuiliwa inaendelea tena bila vikao vyovyote kati ya wazazi, Walimu na bodi za shule. Yanatolewa maamuzi TU. Yasiyojulikana yanatolewa na nani?.
 
Mkuu tunahitaji wazazi kama wewe.
 
Acha uchawi! Acha watoto wasome! An idle mind is the workshop of the devil! Wakati mwingine wakiwa free wanafanya mambo ya hovyo! Wapo wanaojihusisha na kila aina ya uchafu! Wengine mnawang'ang'ania majumbani na kuwalawiti nk nk! Acheni watoto wasome! Tanzania ipo nyuma sana kielimu! Waliotutangulia wanapotembea yatupasa tukimbie!
 
Pamoja upigaji kambi, na hili la michango iliyozuiliwa inaendelea tena bila vikao vyovyote kati ya wazazi, Walimu na bodi za shule. Yanatolewa maamuzi TU. Yasiyojulikana yanatolewa na nani?.
Hizi Kambi si kuna kipindi zilipigwa marufuku?
 
Bila shaka wewe ukiwa ni miongoni mwa hao wajinga kabisa!

Katika suala la elimu hii nchi imeoza!!! Wala si ajabu kukuta mwanafunzi wa chuo kikuu hajui kuandika na bado mnatetea ujinga!

Miongoni mwa watu wanahitaji muda wa ziada wa kujisomea ni pamoja na wanafunzi wanaosoma shule za serikali! Huko kuna ujinga mwingi sana! Acheni watoto wasome!
 
Wewe ndio uache uchawi,nyie ndio wazazi hamtaki kukaa na watoto nyumbani mnawakimbiza bording.

We unadhani kuwabana watoto wakose muda wa kupumzika ndio kuwaepusha na mambo ya hovyo,hujasikia hukohuko shuleni wanafundishwa mambo ya hovyo?
 
Ukiona mtoto wako anahitaji kupumzika ni suala la kuwaambia tu mtoto wangu hatabaki likizo, akirudi ataendelea atakapowakuta wenzake. Shida wazaz sasa hivi tunadekeza sana watoto bila kujua wakati aliopo mtoto wako ni tofauti na ulipokua ww.

Nature ya mitihani inasababisha walimu watumie muda wa ziada na siku za likizo, mfano mtihani wa mock ambao hufanyika may or april maswali yanatolewa mada zote bila kujali hizo mada kama zimemalizika au la.sasa asipofundishwa muda wa ziada hayo maswali atajibuje?

Acheni kulaumu walimu lieni na mfumo wa elimu na mitihani lukuki inayopelekwa mashuleni,mf darasa la saba anafanya upimaji wa awali,pre mock,mock,pre national ,national bado mitihani ya ndani ya shule,bado ya kata sjui klasta.

Hizo mada zitafundishwa saa ngapi na mitihani ni mingi hivyo? jaribuni kufatilia vitu kabla ya kulalamika.
 
Wewe ndio uache uchawi,nyie ndio wazazi hamtaki kukaa na watoto nyumbani mnawakimbiza bording.

We unadhani kuwabana watoto wakose muda wa kupumzika ndio kuwaepusha na mambo ya hovyo,hujasikia hukohuko shuleni wanafundishwa mambo ya hovyo?
Aliyekwambia hatutaki kukaa na watoto nyumbani ni nani? Tunachotaka ni watoto wasome! Iwe kwa kutokea nyumbani ama vinginevyo!

Utakuta unapinga utaratibu huu lakini unaita walimu waje kumfundisha mwanao nyumbani!

Tutengeneze utaratibu mzuri wa kusaidia watoto wapumzike na wasome pia! Muda tulionao ni kidogo sana na mambo ni mengi sana! Ndiyo maana Mh Magufuli alifanya kazi mchana na usiku!
 
Na ndio maana nimesema kupumzika muhimu kipindi cha likizo
 
Wazazi wanaorud usiku nyumbani hawapendi watoto wawepo nyumban kuangalia singeli zenye chura na mitetemo ya matako kwenye tv,ni hatar Kwa makuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…