DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Serikali irekebishe mtaala kama watoto tunawataka wasome muda mchache, kwa schedule ilivyo kwa elimu yetu kwa mwaka ni ngumu kumaliza topics zote with accuracy kwa muda husika..

Kwa ratba ya vipind 5 kwa wiki, approximately dk 200k unataka mtoto amalize syllabus ya physics au biology form 3??? Apo hatujazungumzia advance..

Sometimes shule zetu na walimu wetu wanatafta namna ya kusaidia watoto wetu kwa mazingira ambayo sio rfk af watu tunalaumu tuu...

Kwa primary naweza kukubaliana na nyie ila kwa o level na advanc ni sawa walimu ni sahihi kuwafundsha watoto mpk likizo unless otherwise tubadilishe mtaala ila kwa mtaala huu wa sasa acha wasome
Kama ni kubadilisha mitaala ibadilishwe tu,ila kuwabana watoto namna hii haifai na wala sio afya kabisa,mbaya zaidi inazalisha gharama zaidi kwa mzazi
 
Sambamba na hilo Max, liende pia hili la upigaji wa kambi za kimasomo katika shule ambazo si za bweni!
Pamoja upigaji kambi, na hili la michango iliyozuiliwa inaendelea tena bila vikao vyovyote kati ya wazazi, Walimu na bodi za shule. Yanatolewa maamuzi TU. Yasiyojulikana yanatolewa na nani?.
 
Kuna kijana wangu mmoja yuko la saba, hivi karibuni nikajulishwa hawatarudi mpaka tareh.23; mi nimeona ni vizuri tu kwa faida yake, kwa sababu muda uliobaki ni mfupi sana kwa mtihani, akija nyumbani atachanganya mafaili au kupoteza ile mudi ya kufanya mtihani.

Mwanajeshi ili ashinde vitani, inabidi abaki kambini apate mafunzo, akirudi kwa mkewe alafu kesho aende vitani atashindwa.

Kwa mtazamo wangu mi naona ni wazo jema; hiyo michango midogo isikuumize, bali unawekeza kwa mwanao. Hutaki, muache awe bogus.​
Mkuu tunahitaji wazazi kama wewe.
 
Mheshimiwa Waziri,

Kumekuwa na mtindo wa wamiliki wa shule kuamua tu kwa utashi wao kubakiza watoto shuleni(madarasa ya mitihani) kwa kigezo kwamba wapate muda wa kumalizia mitaala tena bila kushirikisha wazazi huku wakiwa tayari wamepanga na gharama zao.

Hivi walimu wanashindwa vipi kumaliza mtaala kwenye muda uliopangwa?Kibaya zaidi wamekuwa wakiongeza gharama za ziada za Tuition fee na transport hasa kwa shule binafsi.

Sasa kama lengo la walimu ni kumaliza mtaala hili si jukumu lao,kwanini gharama zirudi kwa mzazi?

Je ni sahihi mtoto kusoma bila kupumzika?Kuna watoto wanasoma mbali na wazazi wanahitaji kuonana na wazazi wao ambao hawajawaona kwa muda mrefu,sasa kumshikilia mtoto shuleni muda mrefu kisaikolojia imekaaje?

Mimi binafsi naona shule zimeamua kubuni tu mradi wa kujipatia kipato kwa kigezo cha kumaliza mitaala.

Tayari kuna shule zimeshatoa taarifa kwamba darasa la nne hawatafunga shule ili waendelee kufundishwa,Je mmeruhusu?

Tunaomba hili suala lizuiliwe kisheria na sio kwa matamko ya kila mara maana nakumbuka mwaka Jana ulitoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleni ila naona linajirudia tena.

Pia soma: Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo

Ahsante.
Acha uchawi! Acha watoto wasome! An idle mind is the workshop of the devil! Wakati mwingine wakiwa free wanafanya mambo ya hovyo! Wapo wanaojihusisha na kila aina ya uchafu! Wengine mnawang'ang'ania majumbani na kuwalawiti nk nk! Acheni watoto wasome! Tanzania ipo nyuma sana kielimu! Waliotutangulia wanapotembea yatupasa tukimbie!
 
Pamoja upigaji kambi, na hili la michango iliyozuiliwa inaendelea tena bila vikao vyovyote kati ya wazazi, Walimu na bodi za shule. Yanatolewa maamuzi TU. Yasiyojulikana yanatolewa na nani?.
Hizi Kambi si kuna kipindi zilipigwa marufuku?
 
Ttzo sio wenye shule ttzo ni wazazi
Wazazi weng hawajielew na hawajui kuoji wanaona wenye mashule km miungu mtu
Sababu ayo mambo yote huwa yanafanyika kwenye vikao vya wazazi na shule na wazazi huwa wanakubali wenyewe na ww mzazi mmoja ukisimama kupinga unaonekana km vle ujui kitu hamnazo

Tena izi shule za kidini ndo znaongoza kwa ujinga uwo karo kubwa af ikifka likizo watt wa dlasa la 4/7 wamasema wahamie shule wakae boarding ila wapate mda wa kusoma na kujisomea af tena ikifka likizo wanatwambia tutoe pesa za kuwaudumia watoto wetu wanaobakia mashulen na bado mazazi majinga yanakubali na yanatoa pesa ww mmja ukioji ttzo na mtt wako anaweza akatengwa shulen

Mkitaka kukomesha hii tabia anzeni na wazazi ndo wanakubali ujanga na kuusapoti upuuzi huu wazazi wengi ni wapuuzi na wajinga na wengne bado wanatabia ya kujipendekeza yan karo anatoa ila bado anajipendekeza kwa wakuu wa shule na waalimu

Asilimia 80 % ya wazazi ni wajinga sana x
Bila shaka wewe ukiwa ni miongoni mwa hao wajinga kabisa!

Katika suala la elimu hii nchi imeoza!!! Wala si ajabu kukuta mwanafunzi wa chuo kikuu hajui kuandika na bado mnatetea ujinga!

Miongoni mwa watu wanahitaji muda wa ziada wa kujisomea ni pamoja na wanafunzi wanaosoma shule za serikali! Huko kuna ujinga mwingi sana! Acheni watoto wasome!
 
Acha uchawi! Acha watoto wasome! An idle mind is the workshop of the devil! Wakati mwingine wakiwa free wanafanya mambo ya hovyo! Wapo wanaojihusisha na kila aina ya uchafu! Wengine mnawang'ang'ania majumbani na kuwalawiti nk nk! Acheni watoto wasome! Tanzania ipo nyuma sana kielimu! Waliotutangulia wanapotembea yatupasa tukimbie!
Wewe ndio uache uchawi,nyie ndio wazazi hamtaki kukaa na watoto nyumbani mnawakimbiza bording.

We unadhani kuwabana watoto wakose muda wa kupumzika ndio kuwaepusha na mambo ya hovyo,hujasikia hukohuko shuleni wanafundishwa mambo ya hovyo?
 
Ukiona mtoto wako anahitaji kupumzika ni suala la kuwaambia tu mtoto wangu hatabaki likizo, akirudi ataendelea atakapowakuta wenzake. Shida wazaz sasa hivi tunadekeza sana watoto bila kujua wakati aliopo mtoto wako ni tofauti na ulipokua ww.

Nature ya mitihani inasababisha walimu watumie muda wa ziada na siku za likizo, mfano mtihani wa mock ambao hufanyika may or april maswali yanatolewa mada zote bila kujali hizo mada kama zimemalizika au la.sasa asipofundishwa muda wa ziada hayo maswali atajibuje?

Acheni kulaumu walimu lieni na mfumo wa elimu na mitihani lukuki inayopelekwa mashuleni,mf darasa la saba anafanya upimaji wa awali,pre mock,mock,pre national ,national bado mitihani ya ndani ya shule,bado ya kata sjui klasta.

Hizo mada zitafundishwa saa ngapi na mitihani ni mingi hivyo? jaribuni kufatilia vitu kabla ya kulalamika.
 
Wewe ndio uache uchawi,nyie ndio wazazi hamtaki kukaa na watoto nyumbani mnawakimbiza bording.

We unadhani kuwabana watoto wakose muda wa kupumzika ndio kuwaepusha na mambo ya hovyo,hujasikia hukohuko shuleni wanafundishwa mambo ya hovyo?
Aliyekwambia hatutaki kukaa na watoto nyumbani ni nani? Tunachotaka ni watoto wasome! Iwe kwa kutokea nyumbani ama vinginevyo!

Utakuta unapinga utaratibu huu lakini unaita walimu waje kumfundisha mwanao nyumbani!

Tutengeneze utaratibu mzuri wa kusaidia watoto wapumzike na wasome pia! Muda tulionao ni kidogo sana na mambo ni mengi sana! Ndiyo maana Mh Magufuli alifanya kazi mchana na usiku!
 
Na ndio maana nimesema kupumzika muhimu kipindi cha likizo
 
Wazazi wanaorud usiku nyumbani hawapendi watoto wawepo nyumban kuangalia singeli zenye chura na mitetemo ya matako kwenye tv,ni hatar Kwa makuzi
 
Back
Top Bottom