DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna kijana wangu mmoja yuko la saba, hivi karibuni nikajulishwa hawatarudi mpaka tareh.23; mi nimeona ni vizuri tu kwa faida yake, kwa sababu muda uliobaki ni mfupi sana kwa mtihani, akija nyumbani atachanganya mafaili au kupoteza ile mudi ya kufanya mtihani.

Mwanajeshi ili ashinde vitani, inabidi abaki kambini apate mafunzo, akirudi kwa mkewe alafu kesho aende vitani atashindwa.

Kwa mtazamo wangu mi naona ni wazo jema; hiyo michango midogo isikuumize, bali unawekeza kwa mwanao. Hutaki, muache awe bogus.​
 
Kuna kijana wangu mmoja yuko la saba, hivi karibuni nikajulishwa hawatarudi mpaka tareh.23; mi nimeona ni vizuri tu kwa faida yake, kwa sababu muda uliobaki ni mfupi sana kwa mtihani, akija nyumbani atachanganya mafaili au kupoteza ile mudi ya kufanya mtihani...​
Muda mdogo uliobaki afanye mtihani ni muda gani?
 
Muongozo gani?
Watoto wa wenye mamlaka wanasoma Nje na International schools,unataka wakupangie maisha ya mtoto wako?
Panga mwenyewe,mrudishe nyumbani acheze game likizo yote.
Huu ulimwengu wa kibepari huu, usipopambana na vijana wako, watakuja kuwa wafungua mageti kwa watu.
 
Hivi hao walimu hawana kazi za kufanya wakati wa likizo za wanafunzi? Walimu wa vijijini huwezi kuwapangia kubaki shuleni wakati wana shughuli zao zingine za mashambani.

Kuna kumalizia kuandaa azimio la kazi kwa muhula mpya hiyo kazi hufanyika wakati wa likizo za wanafunzi, sasa kama mwalimu naye yuko shuleni mwaka mzima huo ni ujuha na ulimbukeni wa kazi.

Kama walimu ni mahiri katika kufundisha kwenye vipindi vyao na wanamaliza mada kwa wakati wanafunzi watafaulu tu, sio mpaka wapate matyusheni umiza kichwa wakati wa likizo
 
Hivi hao walimu hawana kazi za kufanya wakati wa likizo za wanafunzi? Walimu wa vijijini huwezi kuwapangia kubaki shuleni wakati wana shughuli zao zingine za mashambani...
Ndio ushangae sasa,ndio maana tunasema ni mradi wa kupiga pesa tu,badala na wao wanaangalie miradi yao huko wanabaki shuleni
 
Ni wakati wa kubadili mfumo wa elimu, ikiwezekana siku za kwenda shule ziwe nne badala ya tano kwa wiki.

Ijumaa iwe ni siku ya michezo tu, pia masomo yawe kwa njia ya vitendo zaidi badala ya rote learning ambayo inadumaza watoto.
Hii ni akili kubwa sana, ulipaswa kuwa waziri wa elimu, decition making zako zingeleta manufaa kwa taifa.
 
Back
Top Bottom