Mkuu asante sana kwa kuleta huu Uzi,wuzara ya elimu na tamisemi wausikie.
Kwanza kabisa nikiri kuwa Mimi ni mwalimu kwa miaka mingi sasa,lakini katika muda wangu wa utumishi kamwe nimekuwa nikipinga sana wanafunzi kubakizwa wakati wa likizo, kufanya hivi kunamnyima mtoto kupata maarifa nje ya elimu ya makaratasi.
Mbaya zaidi wakurugenzi na maofisi elimu wamekuwa chanzo cha mambo haya yote,inafikia kipindi mwalimu ananyimwa likizo kisa tu kufundisha madarasa ya mitihani.
Kwa uelewa wangu mtoto inapofika muda wa likizo huhitaji kupumzika ili kuuandaa ubongo wake kwa yajayo,lakini pia mtoto huwa anatabia ya kumchoka mwalimu,hivyo anapaswa kwenda likizo ili atakapo kutana na mwalimu wake amuone mpya.
Tatizo la mfumo wa elimu yetu unamwandaa mtoto kukalili makaratasi lakini mwisho wa siku hakuna anachokitumia katika uhalisia wa maisha,mfano mzuri ni Mimi mwenyewe,kidato cha nne tulihitimu wanafunzi 250,lakini tuliobahatika kusonga mbele ni wanafunzi 50 tu,je hawa 200 walienda wapi ikiwa muda wao mwingi waliupoteza kusoma makaratasi tu!!?
Wizara husika sikieni kilio hiki ,watoto wapumzike ,na kama wanataka masomo ya ziada basi wakasome najumani kwao kwa utashi wao ila sio kupangiwa shule husika.