Ukiona mtoto wako anahitaji kupumzika ni suala la kuwaambia tu mtoto wangu hatabaki likizo, akirudi ataendelea atakapowakuta wenzake. Shida wazaz sasa hivi tunadekeza sana watoto bila kujua wakati aliopo mtoto wako ni tofauti na ulipokua ww.
Nature ya mitihani inasababisha walimu watumie muda wa ziada na siku za likizo, mfano mtihani wa mock ambao hufanyika may or april maswali yanatolewa mada zote bila kujali hizo mada kama zimemalizika au la.sasa asipofundishwa muda wa ziada hayo maswali atajibuje?
Acheni kulaumu walimu lieni na mfumo wa elimu na mitihani lukuki inayopelekwa mashuleni,mf darasa la saba anafanya upimaji wa awali,pre mock,mock,pre national ,national bado mitihani ya ndani ya shule,bado ya kata sjui klasta.
Hizo mada zitafundishwa saa ngapi na mitihani ni mingi hivyo? jaribuni kufatilia vitu kabla ya kulalamika.