Waziri wa Elimu kama kazi imemshinda ajiuzulu, walimu shule binafsi wanalipwa mishahara finyu na hasemi chochote

Kuna ulazima wa wizara hii kujitafakari pamoja na taasisi zake. Binafsi namuomba mheshimiwa Rais asuke upya hii wizara. Sioni hata ile miaka mitano iliyopita ni kipi cha kijivunia. Naandika nikiwa na akili timamu na pia ni msomi mubobezi wa shahada ya juu juu zaidi. Tuweke siasa pembeni, hii wizara namuomba mheshimiwa Rais aitizame upya kabisa kabisa kabisa. Naamini wadau wa elimu wakiulizwa wana mengi ya kuzungumza.
 
Usiwe na mawazo ya kijinga namna hii. Kama halikuathiri wewe linamuathiri nduguyo. Ni muhimu sheria ya ajira ifuatwe, kama wamiliki hawawezi , basi wasianzishe hizo shule. Sio kuwageuza watanzania wenzao watumwa.
 
Sio kuwageuza watanzania wenzao watumwa.
Utumwa huu unaendelezwa na sera mbovu za serikali ya ccm. Kama yenyewe imewatelekeza unataka mm watu binafsi wafanyeje? Wewe chukia, foka ama tukana lkn huu ndiyo ukweli.
 
Kama ipo ivyo acha iyo kazi mkuu lakini sio kuja na agenda ya kumuondoa waziri wa elimu ofisini.
 
Ungeweka na mfano wa shule ingekuwa vema.

Hivi vyama vya wafanyakazi ndio vyakulaumiwa, vimekaa kimya wakati wanachama wake wananyanyasika.

Waziri unamlaumu bure.
Walimu wengi wanaofanya kazi shule za private hukataa kujiunga na vyama vya wafanya kazi kwaio.if am not mistaken watakua sio member wa chama Cha walimu
 
Kwenye issue za simu me nafikiri ukipewa ajira kila sehemu Ina utaratibu wake Kama hawataki uchat inabidi ukubali .tujikite kwenye swala la maslahi tu
 
Shule nyingi za private zinamlipa mwalimu kulingana na uwezo wake kwenye delivery ya materials kwa wanafunzi ukiwa jembe hawawezi kukulipa kizembe.unafundisha SoMo lako linafanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa wakulipe Tsh150,000/= haiwezekani Ila ukiwa mwalimu mzembe wanakulipa kizembe.
 
Corrections:
1. Entervene[×] Intervene[√]
2. Dwimdle[×] Dwindle [√]

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli manyanyaso ni mengi mno.
Ila kuhusu kuoa au kuolewa mmekubali wenyewe.Oeni watoto wao au muwaoe wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…