kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
Waziri wa elimu hebu litupie macho hili la walimu kuwaadhibu wanafunzi kukosa michango na mahitaji ya shule,kama hao watoto ndio watafutaji wa hayo mahitaji.
Kwanini usimuite mzazi ukamuadhibu kwa hilo kosa la kutomtimizia mtoto wake mahitaji, unamchapa viboko mtoto ana kosa gani?
Pili hiyo michango ni ya nini, nasi tunaambiwa elimu ni bure. Hao waalimu wa sayansi wa kujitolea kwanini wasiajiriwe huko.
Kwa kweli mnazingua watoto mwisho wa siku wakichoka viboko, watoto kiume wanaingia mitini kwenda kuvuta ngada na wakike wanakwenda kupewa mimba hebu kuweni makini kidogo kuwaelimisha na kuwasimamia hao walimu wenu wahuni.
Tunazalisha taifa la namna gani 2025 sio mbali mjue!