Waziri wa Elimu simamia utawala katika vyuo. Wanafunzi wanaumizwa na elimu inaanguka!

Hapo ukiriguru -Mwanza siyo kweli jombaaa hakuna mwalimu kijana pale isipokuwa tu yule mkuryaa nae age imeenda
 
Nilipoona kichwa cha habari nilidhani unazungumzia taaluma inayotolewa labda haikidhi mahitaji ya soko la ajira!
Kumbe ni masuala ya upendeleo ktk utoaji wa alama, rushwa za ngono na mahusiano kati ya walimu na wanachuo.

Kusemaukweli binafsi huwa naamini kama mwanachuo anajiamini kwamba, anaweza kupata alama zinazotakiwa, basi hawezi kushawishika kutoa rushwa ya aina yoyote ile.
Tatizo kubwa la vyuo vya juu, ni kuruhusu masuala yote ya mtaala kuwa chini ya chuo husika.
Nadhani wizara ilitakiwa kuweka utaratibu wa kukagua kozi zinazotolewa na kila chuo, na pia kufuatilia uhalali wa ufaulu kwa vyuo husika.

Kuna vyuo wanasoma mambo mengi kwa muda mfupi mfano UDOM, na wakati vyuo vingine wana mada chache japo kozi zinafanana.
Upimaji nao pia huwa tofauti. Jambo linalosababisha elimu kuwa kama vita. Na matokeo yake ndio hayo kwa baadhi ya wanachuo kutafuta kamserereko, kwa kukubaliana na hayo yaliyosemwa kwenye andiko hili!
 
Mleta mada bila kuweka ushahidi wa tuhuma zako wazi. Binafsi ninakubakisha katika sehemu ya kundi lenye nia ovu ya ku katisha tamaa malekichara na matutorio, na mainstrakta ili wafanye kazi kwa uoga. Hata hivyo, ninavyowajua hao wafanyakazi wa vyuo wataendelea kusimamia weledi ili kuliokoa taifa.
 
Ni nchi gani wanasahihisha mitihani ya chuo Kikuu kwa utaratibu huo?
 
Kozi zote zinazofundishwa vyuo vijuu lazima zipitishwe TCU waziaprove. Na Kila baada ya miaka mitatu zinakuwa reviewed.
Halafu pia lazima external examiner apitie mitihani aone kama iko chini ya kiwango. Wizara si ya kulaumu imeweka mifumo mizuri labda kama ufanyaji kazi wa hiyo mifumo ndio tatizo.
 
Mzumbe Morogoro campus Hali ikoje? Mleta mada hebu funguka hapa.
 
Hayo mambo ya kutaka ushahidi ndo yanasababisha mitaani tunawachoma moto vibaka. Tuko mitaani na wengine ni wazazi na wengine ni wahitimu au wanafunzi. Tukisema unasema lete ushahidi, wakati huo muhusika pia anajitahidi kuficha ushahidi. Sasa hivi hata viongozi wa dini wakituhumiwa wanadai ushahidi wakati wao wanafundisha yasiyo na ushahidi.
 
Hao TCU waropokaji tu! Ni wale wale toka vyuoni, eti wakifika TCU wanakuwa wajuzi kuliko wengine. Kila siku wanakopi ya nchi zingine, bureeee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…