MANYORI Jr
JF-Expert Member
- Mar 25, 2012
- 462
- 343
Ndugu wana Jf ,habari za wakati huu na hongereni kwa kuuona mwaka mpya 2021.Nami pia ninawatakieni kheri ya mwaka huu!
Hili ni chapisho langu la kwanza kwa mwaka huu 2021 tangu nilipoonekana humu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Kama mada yangu inavyojibeba kupitia jina lake,ningependa kueleza kwa kina kwa nini ninawaomba watu hawa wakubwa kufanya vile.
Kwenye tasnia ya elimu(education industry) hapa nchini kwetu panatambulika mifumo miwili tu ya utolewaji na upatikanaji wa elimu(msingi hadi chuo kikuu)ambayo ni;Mfumo rasmi na Mfumo huria au usio rasmi.
Kwa manufaa ya ufahamu,mfumo rasmi hutekelezwa kupitia taasisi maalumu zilizotengenezwa kwaajili hiyo(yaani shule au vyuo) ambavyo umiliki wake unaweza kuwa chini ya mtu binafsi ama umma(serikali). Watu wanaopitia mfumo huu ili kupata elimu hulazimika kufuata utaratibu maalumu na vigezo maalumu vikiwemo ufaulu katika ngazi za kitaaluma zilizotangulia pamoja na muda maalumu(Miaka 7 msingi,Miaka4 na 2 Sekondari n.k). Watu wa mfumo huu huchaguliwa na Serikali na pia Shule binafsi huruhusiwa kuwapokea(kwa mujbu wa vigezo vyao wao kama wao) na mara nyingi wanakuwa na umri maalumu pia kwa ngazi za awali hasa msingi na sekondari.
Mfumo huria katika nchi yetu ulianzishwa kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa huduma ya elimu kwa watu wote ambao vigezo vilivyo katika mfumo rasmi hawakuwanavyo kwa sababu mbalimbali kama vile kuugua muda mrefu,kupata ujauzito,kufukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu na muhimu zaidi kutokukidhi ufaulu wa kiserikali bila kusahau kuishi na jamii inayokuwa changamoto kwenye elimu yao.Watu wote hawa wanapewa dirisha la pili(second chance) kuthibitisha kuwa wanaweza kuipata elimu.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imepewa jukumu la kuratibu mfumo huu wa elimu yetu kwa kuzitambua, kuzihakiki, kuzisajili na kuzisimamia shule huria(Open Schools) zote nchini ambazo ndizo wakala anayetambulika kisheria kutoa huduma ya elimu ya Masafa na Ana kwa ana yaani ODL kama wanavyouita.
Shure huria (Open Schools) zinategemea hasa watu waliotemwa na mfumo rasmi kuwa wateja(wapokea huduma) wao na huwa na bei ndogo sana (makadirio ya 140,000/= hadi 350,000/=) kama ada kwa mwaka.
Watu wanaopitia mfumo huu huria wamepewa vigezo kadhaa ili kuunganishwa katika mfumo rasmi kwenye ngazi ya Form Five &Six kama vile umri usiozidi miaka 25 ,kufanya mtihani wa QT na Mock ya Kimkoa inayoratibiwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Makao makuu na Kufaulu vizuri Mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne.
Shule huria zote zipo chini ya Maafisa Elimu ya Watu Wazima ngazi ya Wilaya na Wakufunzi Wakazi ngazi za mikoa. Kutokana na hili, shule huria zimewekwa maalumu kwa watu waliokosa fursa katika mfumo rasmi!
Katika siku za hivi karibuni, wakuu wa shule za serikali zilizo mijini(wilayani na mikoani) hapa nchini wamekuwa wakihujumu miundombinu,raslimali watu na nia njema ya serikali yetu tukufu ya kuanzisha shule huria (Open Schools) ninazosajiliwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ili kuwawezesha walengwa kupata elimu katika mfumo huria kwa kuwa hawakidhi vigezo vya mfumo rasmi kutokana na kuendesha huduma hizo katika shule za serikali zilizo katika mfumo rasmi ambazo pia hazijasajiliwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kutoa huduma ya elimu kwa watu waliokosa fursa katika mfumo rasmi.
Wakuu hawa wa shule za serikali na hata binafsi wamekuwa wakiwatoza pesa walengwa (watu wanaopaswa kuwa katika mfumo huria kupitia Open Schools nchini) kati ya Sh.100,000/= hadi 140,000/= kama ada kwa mwaka.Wakuu hawa huwachanganya pamojavwatu hawa waliokosa sifa katika mfumo rasmi na wale waliokidhi sifa za mfumo rasmi katika madarasa yaleyale kinyume na taratibu za uendeshaji wa shule za serikali na utolewaji wa elimu kwa kupitia mfumo huria.
Jambo hili ni hatari sana kwa kuwa linaondoa kusudi la serikali kuwachuja na kuwachagua wanafunzi inaowataka kupitia vigezo na sifa zake ili wajiunge na shule za sekondari za serikali.
Ada inayotozwa na wakuu hawa wa shule haiendi serikalini kwa kuwa shule hizo hazijasajiliwa wala hazitambuliki kuwa zinatoa huduma hii na kwa hivyo hii pesa inaishia kwao wao na vibaraka wao wakati huohuo Shule huria zinakosa wateja(wanafunzi) kutokana na jamii kuhadaika na miundombinu ya shule za serikali na imani juu ya mamlaka za kiserikali bila kujali iwapo shule hizi za serikali ni mahsusi kwaajili ya watu wa aina ipi au mfumo upi na iwapo zinatambulika na mamlaka kuwa zinatoa huduma hiyo.
Kutokana na jambo hili, wazalendo wenzetu ambao kwa dhati ya mioyo yao waliamua kujiajiri na kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuhakikisha panakuwepo na elimu bila kikwazo kwa kuanzisha shule hizi huria na kusajiliwa na Taasisi ya Watu Wazima wanalia na kusaga meno!
Wanalia kwa kuwa wakuu wa shule za serikali za mijini ambao kimsingi ni "Wahujumu Uchumi" wameamua kuingia katika biashara bila hata kutambuliwa na mamlaka na hivyo kuisababishia serikali upotevu ma mapato ya mamilioni ya fedha ambazo zingepatikana iwwapo watu waliohadaiwa na wakuu hawa wangejiunga na Open Schools.
Nimalizie kwa kusema kwamba, Waziri wa Elimu, Waziri wa OR-TAMISEMI na Mkurugenzi Wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wanapaswa kulilinda soko la shule huria nchini kwa kuhakikisha kuwa shule zote za serikali na zile za binafsi ambazo hazijasajiliwa kutoa elimu kwa mfumo ODL zinaacha mara moja kuwapokea na kujifanya zinawasajili watu wanaohitaji huduma za elimu kwa mfumo wa ODL.
Zaidi ya hili, wawatumbue wakuu wote wa shule za serikali nchini ambao tayari hadi wakati huu wako bize kupokea wanafunzi walioshindwa kutimiza vigezo katika mfumo rasmi ili wajiunge pamoja na wanafunzi wa mfumo rasmi sambamba na kuzipiga faini shule binafsi ambazo pia zimekuwa zikifanya hivi kinyume kabisa ba utaratibu. Maafisa Elimu ya Watu Wazima(W) na Wakufunzi Wakazi(M) wajitafakari iwapo wanachokisimamia ndicho wanachokiona kinafanyika.
Ahsanteni sana!