Waziri wa Elimu wekeni matokeo kwa majina ya form four

Waziri wa Elimu wekeni matokeo kwa majina ya form four

God Fearing Person

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2020
Posts
767
Reaction score
2,570
Ili tuone unaupiga mwingi ebu weka matokeo kwa Majina ndo tuamini upo serious na Kazi yako.

Watoto huku uswahilini wanataja taja tu namba za uongo wakati wamepata zero na mbaya wanadanganya wazazi wao.
 
Ili tuone unaupiga mwingi ebu weka matokeo kwa Majina ndo tuamini upo serious na Kazi yako.

Watoto huku uswahilini wanataja taja tu namba za uongo wakati wamepata zero na mbaya wanadanganya wazazi wao
Inabidi wazazi waende na muda, wajue kutumia tovuti na mtandao kwa ujumla. Hakuna haja ya kuweka majina, ni wazazi waende na wakati, namba tu inawashinda kuijua, wanaweza kufuatilia maendeleo ya watoto kweli?!
 
Utaratibu ulibadilika sababu Mwanaisha kipindi kileee, aliandikwa sana. Wacha namba ziendelee.
 
Acha umbea Ile iliwaletea watoto stress mtaa mzima wanajua matokeo Yako Bora wanavyoweka no. hakuna mzazi atataka kujua matokeo ya mwanae ashindwe labda kama mzazi hauko makini
 
Ili wagundue nini? Matokeo ni siri, mhusika pekee ndo anapaswa yajua
 
Back
Top Bottom