Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Serikali kupitia Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) inatarajia kuwasilisha Bajeti Kuu ya Mwaka wa Fedha 2026/27 leo Alhamisi Juni 11, 2026 Bungeni Jijini Dodoma.
Balozi Khamis Mussa Omar alinukuliwa akisema bajeti hiyo itatumika kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2026/27–2030/31) pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025-2030.
Unatarajia nini kutoka katika bejeti hiyo?
Updates
Katika kuendeleza matumizi ya mafuta ya kula yanayozalishwa kwa kutumia mbegu za ndani ya nchi, Waziri wa Fedha amezitaja hatua zingine zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na:

- Msamaha wa VAT: Serikali itaendelea kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mafuta ya kula yanayozalishwa nchini kwa kutumia mbegu zinazoshwa ndani ya nchi.
- Ushuru wa Mafuta Safi: Serikali itaendelea kutoza ushuru wa 35% au Dola za Kimarekani 300 kwa kila tani moja ya mafuta safi ya kula kutoka nje (refined oil), ikitegemea kiwango kipi kitakuwa kikubwa zaidi.
- Kanuni Mpya za Uagizaji: Serikali imeandaa kanuni mpya za uagizaji wa mafuta ya kula ili kudhibiti uingizaji wa bidhaa hiyo nchini na kukuza tasnia ya ndani.
- Utoaji wa Vibali Maalum: Kupitia Wizara ya Kilimo, serikali itatathmini na kutoa vibali maalum kwa waagizaji wa mafuta baada ya kujiridhisha juu ya uwekezaji wao katika uzalishaji wa mbegu za alizeti, pamba, na michikichi chini ya kanuni za COPRA za mwaka 2026.