Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu ninaomba ufafanuzi wako kidogo juu ya Makato ya Vocha

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu ninaomba ufafanuzi wako kidogo juu ya Makato ya Vocha

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
DKT MWIGULU, WAZIRI WA FEDHA NINAOMBA UFAFANUZI KIDOGO JUU YA MAKATO YA VOCHA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kwanza Mhe Waziri nikupongeze kwa hotuba YAKO nzuri ya Bajeti. Mimi si mchumi, lakini niliisikiliza na nimeisoma nimeona ni bajeti ambayo inagusa maisha halisi ya Mwananchi. Ni bajeti ambayo inaenda kumkomboa Mwananchi ktk sekta ya Afya, miundombinu, Elimu, Kilimo n.k.

Leo si nia yangu ya kuichambua bajeti ila ninataka nipate maelezo kidogo juu ya makato ya vocha. Ulisema hata Wabunge hili jambo hawalielewi vizuri, lakini Mimi baada ya ufafanuzi wako nilikuelewa. Lakini Nina maswali kidogo ambayo ninaamini unaweza kutupa ufafanuzi.

Mhe Waziri ulisema mtu akiweka kwenye simu Tsh 1,000/= anaweza kukatwa Tsh 10/= Sawa! Lakini Mhe Waziri vifurushi vingi vya watu wa chini ni 500/=, 1,500/=, 2,000/= n.k

Kwa tafsiri rahisi mtu anayetaka kujiunga kifurushi Cha 1,000/= itamlazimu anunue vocha ya Tsh 1,500/= kwani akinunua vocha ya Tsh 1,000/= akisha katwa Tsh10/= inabaki Tsh 990/= ambayo haiwezi kununua kifurushi tena lakini akinunua vocha ya Tsh 1500/= akikatwa Kodi atabakiwa na Tsh 1490/= ambapo itamlazimu kununua kifurushi Cha Tsh 1,000/= kwani cha Tsh 1,500/= pesa haitoshi. Na ubaya zaidi itakayobaki kwenye simu Tsh 490/= mitandao wanaichukua kwa kukutumia sms za hovyo hovyo na nyimbo ambazo hata hujaomba.

Mhe Waziri Dkt Nchemba ninajua wewe ni msomaji mzuri na hili utaliona na utatupa ufafanuzi.


Ushauri wangu ni kuwa pamoja na nia hiyo njema,basi wewe Waziri wa Fedha, Waziri wa Mawasiliano Dkt Ndungulile, Watu wa Mawasiliano na Makampuni ya Simu basi mkae, mkubaliane bili kifurushi kilichokuwa kinapatikana kwa Tsh 1,000/= basi kipatikane kwa Tsh 990/= fedha inayobaki baada ya makato ya Tsh 10/= kutoka kwenye vocha ya Tsh 1,000/=. Hii itaondoa gharama ya kununua vocha ya 1,500/= wakati lengo Langu ni kununua kifurushi Cha 1,000/=.

Maelezo yangu haya nimetumia mtandao wa Vodacom kama sampling.

Ningekuwa Bungeni ningemalizia kwa kuunga mkono hoja, huku nikisema serikali itoe ufafanuzi au kuchukua mapendekezo yangu. Ahsante sana!
 
Back
Top Bottom