Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu: Pato la Taifa (GDP) lakua hadi 5.5% mwaka 2024, mfumuko wa bei wabaki imara
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka 2024 umefikia asilimia 5.5, ukilinganishwa na asilimia 5.1 kwa mwaka 2023 na asilimia 5.4 kwa mwaka 2022.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha mwaka 2025/26 Bungeni leo Juni 4 ameongeza kuwa, katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025, mfumuko wa bei nchini umefikia wastani wa asilimia 3.1, ukilinganishwa na asilimia 3.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2023/24.
Dkt. Nchemba amesema kuwa wastani huu wa mfumuko wa bei ni thabiti na imara zaidi ikilinganishwa na nchi jirani katika ukanda huu.