Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Duh! Utafikiri Tanzania wanatengeneza magari. …Shida ya kuongozwa na zero brain ndio hii. Watanzania mtapigika sana hadi mtaita maji mma msipochukua hatuaWaziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 bungeni Juni 11, 2026, ametangaza kupandishwa kwa viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini, huku kigezo cha umri wa gari kikichukua nafasi kubwa.
Katika mabadiliko hayo, magari yenye umri wa kuanzia miaka 8 hadi 10 yamepandishwa ushuru kutoka asilimia 15 ya sasa hadi asilimia 20. Kwa upande wa magari yenye umri wa zaidi ya miaka 10 lakini hayazidi miaka 20, ushuru wake umepandishwa kutoka asilimia 30 hadi asilimia 40.
Kasi hiyo ya ongezeko imegusa pia magari chakavu zaidi, ambapo Mhe. Balozi Khamis amebainisha kuwa magari yenye umri unaozidi miaka 20 na kuendelea sasa yatatozwa ushuru mkubwa wa bidhaa wa kiwango cha asilimia 50.
Akitolea ufafanuzi lengo la hatua hiyo, Waziri wa Fedha ameeleza kuwa mbali na kuongeza mapato ya serikali, mkakati huo unalenga kupunguza uingizaji wa magari hayo mabavu ambayo yamekuwa yakisababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kupitia uzalishaji wa taka ngumu, ambazo zimekuwa zikitumia gharama kubwa kuziteketeza.
Mhe. Balozi Khamis amelihakikishia Bunge kuwa hatua hizo mpya za ushuru wa bidhaa kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 355.09.
Hayo ni makaratasi tu, katika uhalisia, ukiagiza gari jipya ushuru ni mkubwa ajabu. Ni Afadhali uagize gari la miaka 20 kuliko la miaka 3 kwa hela TRA watakazokutoaHawana AKILI KABISA Hawa yaani wanawazaga humo humo tu hawatoki ndani ya box.
Duu kazi ipo.Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 bungeni Juni 11, 2026, ametangaza kupandishwa kwa viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini, huku kigezo cha umri wa gari kikichukua nafasi kubwa.