Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba umesikia ujumbe wa mafao Bungeni Dodoma?

Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba umesikia ujumbe wa mafao Bungeni Dodoma?

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Mhe. Mwigulu Nchemba Waziri wa fedha lazima ufahamu kuwa wanaostaafu leo ni Kaka zako, Ndugu zako na dada zako pia waliostaafu siku nyingi wengine ni Baba zako wadogo na ndugu wa damu.

Nikushauri tu, achia pesa watu walipwe, miradi ina umuhimu pia wastaafu wanahitaji waishi maisha yao.

Hutakuwa na Baraka kwenye kiti hicho endapo utaendelea kutowathamini hao wastaafu na kujua ni haki yao. Kumbuka hao wengi wao ni askari Polisi.
 
Shetani hawezi kusikia mambo ya Mungu, hapo umechemsha. Shetani?
 
Ni vigumu kunishawishi kuwa evolution ya ubinadamu ya mwendazake ilikuwa imekamilika. Alikuwa na ukatili beyond humanity. Utamwibiaje mstaafu hela yake kwa kisingizio cha kufanya mambo ya hovyo?
 
Ni vigumu kunishawishi kuwa evolution ya ubinadamu ya mwendazake ilikuwa imekamilika. Alikuwa na ukatili beyond humanity. Utamwibiaje mstaafu hela yake kwa kisingizio cha kufanya mambo ya hovyo?
Eti hela ya mtu ipelekwe kwenye miradi
 
Kwakweli hii haiko fair kabisa,MTU hela ni zako umezitolea jasho na pengine ulijinyima ili mwisho wa siku hizo pesa zije zikusaidie lakini watu wasio na huruma ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao wanaona fedha zako kama ndio sehemu ya kutatua matatizo waliyoyashindwa.

Fedha zangu si mnilipee? Nilipe nisepe bhanaaa...wakati mm nafanya kazi ww ulikuwa kijijini kwenu huko,pangia majukumu pesa zako achana na zangu kabisa.

Wakati mwingine Serikali inajitafutia manuksi kwa sababu ya wizi wa wazi kabisa kama huu.

Kodi unakusanya

Ushuru unakusanya

Tozo unakusanya

Bado kuna Maservice levy,Usafi,mshikamano,uzalendo zote hizo hazikitoshi tu mpaka uchukue pesa za mishahara ya watu waliokatwa kwa matumizi ya baadae?

Misaada nje unapewa,mikopo unapewa,sijui kwann serikali hairidhiki hadi ichukue pesa za wafanyakazi?
 
Mhe. Mwigulu Nchemba Waziri wa fedha lazima ufahamu kuwa wanaostaafu leo ni Kaka zako, Ndugu zako na dada zako pia waliostaafu siku nyingi wengine ni Baba zako wadogo na ndugu wa damu.

Nikushauri tu, achia pesa watu walipwe, miradi ina umuhimu pia wastaafu wanahitaji waishi maisha yao.

Hutakuwa na Baraka kwenye kiti hicho endapo utaendelea kutowathamini hao wastaafu na kujua ni haki yao. Kumbuka hao wengi wao ni askari Polisi.
@Mwigulu Nchemba
 
Back
Top Bottom