Waziri wa Fedha na Mipango ateuliwe Profesa Musa Assad

Waziri wa Fedha na Mipango ateuliwe Profesa Musa Assad

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Ikimpendeza Mheshimiwa Rais, anaweza kumteua Prof. Assad kuwa Mbunge na kisha kuteuliwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Sina shaka na utendaji wake hasa akiwa CAG, alisimama imara hali iliyompelekea kukumbwa na mizengwe ya wachumia tumbo.

Umri hauwezi kuwa kikwazo sababu tuna Mawaziri wengi wenye umri mkubwa zaidi yake.
 
Point huyu Asaad arudi Tu hakuna namna. Uadilifu wake ni WA kiwango cha juu.
 
Katiba hairuhusu CAG aliyeko madarakani ama aliyestaafu kushika wadhifa wowote ule wa utumishi. Means prof Assad hawezi kushika madaraka yyt ndani ya utumishi
 
Mleta mada inaonekana uelewa wako ni mdogo sana sana!!

Soma katiba ya nchi kuhusu CAG, sio kukurupuka

Ingekuwa ni hivyo udhanivyo basi Ludovick Utoh angekuwa na wadhifa hata wa ubalozi
 
Unaijua Definition ya Utumishi kwa muktadha uliotumika?

Mtumishi wa Umma kwa mujibu wa Katiba ana sifa zake
Mf.Mbunge si mtumishi wa Umma japo anakula Mshahara so unapaswa kujiuliza Waziri ni mtumishi wa Umma?

Kiongozi wa Watumishi wa Umma kwa mujibu wa Katiba ni Katibu Mkuu Kiongozi, jee Mawaziri wapo chini ya Chief Secretary? Anzia hapo kwanza …
Katiba hairuhusu CAG aliyeko madarakani ama aliyestaafu kushika wadhifa wowote ule wa utumishi. Means prof Assad hawezi kushika madaraka yyt ndani ya utumishi
 
Itakuwa bomba apewe uPM LOL! Kama namuona vile ndugai
1617112281499.jpeg

Mleta mada inaonekana uelewa wako ni mdogo sana sana!!

Soma katiba ya nchi kuhusu CAG, sio kukurupuka

Ingekuwa ni hivyo udhanivyo basi Ludovick Utoh angekuwa na wadhifa hata wa ubalozi
Hivi lengo lilikuwa ninini hasa? Naona kuna shida mahali. Kwanini Katiba iwa-limit sana ma-CAGs' kuhusu kutoshika madaraka ya Utumishi bada ya kustaafu??
 
Ikimpendeza Mheshimiwa Rais, anaweza kumteua Prof. Assad kuwa Mbunge na kisha kuteuliwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Sina shaka na utendaji wake hasa akiwa CAG, alisimama imara hali iliyompelekea kukumbwa na mizengwe ya wachumia tumbo.

Umri hauwezi kuwa kikwazo sababu tuna Mawaziri wengi wenye umri mkubwa zaidi yake.
Siku Chadema ikishika dola ndipo atakuwa waziri wa fedha na mipango! Kwa sasa haiwezekani alinyea kambi
 
Laiti kama kwenye Katiba yetu mngejua nafasi/nguvu/heshima aliyokuwa nayo/aliyopewa CAG awe madarakani/kastaafu basi mngeacha kujitesa na Kupiga hizi RAMLI ambazo hazitakuja kutokea mpaka pale Mwana wa adamu atakapokuja.. Hebu tumuombeeni mapumziko mema CAG Prof Assad na familia yake..
 
Ateuliwe tu, akikataa apelekwe wizarani kwa pingu
 
Back
Top Bottom