Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Ulichokiandika nadhani sio, wewe kama uko kwenye msiba inakuwaje unaanza kujibizana kwenye mitandao, andika mambo ya msingi msiba usiwe kisingizio, kama unachosema kina mashiko kwanini ameapishwa Rais si tungesubiri JPM azikwe? aacha visingizio Katiba iko hai
 
Tuandikie ibara tafadhali. Mambo yanakwenda kwa sheria, nipo tayari kukuunga mkono kama utaandika kama mtoa Thread, kapanga na kuonyesha katiba inasemaje?

Mi si mpenzi wa mtoaji threada lakini kwa udadafuaji alioufanya nampa 5.
Kwamba Rais ni taasisi unataka upewe ibara?
 
Kweli aliye mwita Mwigulu hajakosea. Phd holder hajawaelewa TLS. Au hakusoma bandiko lote? Au ni wale wale mawaziri viherehere wa mtandaoni?
Mbona bandiko la Tls liko wazi kabisa? Kweli hii nchi ina vihiyo wengi. Ina kuwaje mtu ana Phd anashindwa kuelewa bandiko la kurasa moja? Au ni zile phd za mtaani?
Ni aibu mtu kama huyu kupewa madaraka. Au amesha panic kwamba Mh. Mama Samia akivunja baraza hata mchukua? Maana najua viherehere kama huyu labda alikuwa akimdharau Mama Samia sasa hana pa kushika.
Mwigulu kuwa mpole, Mama ni mtu mwema, haweki kinyongo. Sana sana kita kutesa wewe mwenyewe. Dharau ulizo muonyesha yeye wala hazikumbuki.
 
Kuna watu wanapima upepo nadhani sidhani kama wana nia Njema na Ta if a hilii.
 
Mwigimulu si mwanasheria
 
Nchi haiendeshwi kwa taratibu za kimila. TLS wao wamehadharisha tu muwe makini msikurupuke.
Si mara moja uongozi uliopita umekuwa ukikiuka katiba au anataka iwe mazoea? Mliwahi kuteuwa wabunge wa kiume wengi zaidi ya wanawake. Wanaharakati na wapinzani waliwashitukia na kuteka katiba ifuatwe. Posi alitolewa ubunge na kupewa ubalozi ili kukuwa soo.
Wameteuliwa mawaziri wawili bila kuwapo kwa waziri mkuu kinyume cha katiba. Kwa kuwa hakuna aliyewashitua katiba ilikanyagwa.
Mara ngapi wabunge wasio na chama wamekuwa wakishiriki Bunge kinyume cha katiba? Au unafikiri tunafurahi?
Leo TLS imewahadharisha unang'aka. Tuache kudharauliana.
 
Mwigulu ana hoja,ajibiwe kwa hoja pia.Sio kunza kumkashifu
 
Uchambuzi huu wa Katiba ndio unatoa tafsiri sahihi ya ukomo wa Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri kutokana na kifo cha Rais wa nchi aliyekuwa madarakani.

Wenye hoja/mtazamo tofauti, kwenye mjadala huu, wana lengo ovu la kupandikisha chuki katika jamii.
 

Amesahau kuwa aliteuliwa kabla ya maziko ya marehemu Agustino Mahiga.
 
TLS walitoa hoja zao kwa vigezo vya kikatiba na kisheria.

Mwigulu ame manipulate vifungu vya katiba kwa faida ya kisiasa kwake yeye binafsi kwani hana uhakika wa kurejeshwa mama akivunja baraza..... which she will do, much to the chagrin of Mwigulu & co!

Mwacheni mama afanye kazi. Kumbuka naye atakuwa anafanya kazi yake kipindi hiki with one eye on the 2025 presidential contest. So, najua yule mama yupo smart - smart enough kuweza kutumia state apparatus at her disposal katika kuhakikisha potential presidential contestants wengine kama Mwigulu wanakuwa weakened as much as possible in the public eye.... moja ya strategy kufanikisha hili inaweza kutokuwapa kina Mwigulu nafasi za uteuzi ambazo definetely zinaweza kuwapa umaarufu.

Kwako comrade Mwigulu Nchemba
 
Nimesoma mwongozo uliotolewa na chama cha wanasheria Tanzania bara( Tanganyika Law Society)* ambao umesainiwa na Rais wa chama hicho Dr Rugemeleza Nshala

Mwongozo huo unajibu swali lifuatalo

Je, Katiba inalazimisha au inamtaka Rais aunde na aapishe Baraza la Mawaziri pindi atakapotwaa madaraka baada ya Rais kufariki dunia?

Ukisoma katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977 kwenye ibara ya 37( 5) imeeleza kuwa, endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais aliyeko madarakani kupoteza sifa za kuwa Rais ikiwemo kufariki dunia, basi makamu wa Rais ataapishwa na kuwa Rais mpya wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Je, baada ya makamu wa Rais kuapishwa na kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baraza la mawaziri linakuwa limevunjwa?

Jibu la hilo swali ni HAPANA, baada ya makamu wa Rais kuapishwa na kuwa Rais, baraza la mawaziri la awali, bado linaendelea kama kawaida, kwa maana ya waziri mkuu, mawaziri na wajumbe wengine wanaendelea na nyadhifa zao kama kawaida.

Kwa nini?

Kwa sababu, ukisoma katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, kwenye ibara 42(5), inaeleza aina ya watu wanaoweza kuapishwa na kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania

Ibara hiyo ya 42(5), inasema " Kila Rais mteule na na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais, kabla ya kushika madaraka yake, ataapa mbele ya jaji mkuu wa jamhuri ya muungano "

Kwa hiyo hapo kwenye hiyo ibara ya 42(5), inaeleza kuna aina 2 za watu wanaoweza kuapishwa na kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania

1. Rais mteule, ambaye huyu amefafanuliwa vizuri kwenye ibara 42(1) ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake

2. KIla mtu atakayeshika madaraka ya Rais,ambaye huyu amefafanuliwa kwenye ibara ya 37(3) ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ambao ni wafuatao kwa kufuata mtiririko kutoka juu.

a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

b) Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

c) Jaji Mkuu wa mahakama kuu ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania

Kwa hiyo sasa ni Rais mteule tu, ambaye ameshinda uchaguzi mkuu wa Rais na kutangazwa mshindi na tume ya taifa ya uchaguzi( NEC), ndiye akiapishwa kushika madaraka yake, waziri mkuu, mawaziri, Naibu mawaziri na mwanasheria mkuu wa serikali wote wanakoma kuendelea na nyadhifa zao, na hiyo imeelezwa kwenye ibara ya 51(3)(a) na ibara ya 57(2)(f) ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977

Lakini makamu wa Rais au Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania au Jaji mkuu wa mahakama kuu ya jamhuri wa muungano wa Tanzania, endapo watatokea kuapishwa na kuwa Rais kwa sababu yeyote ile iliyotokana na Rais aliyeko madarakani kupoteza sifa za kuwa Rais, basi waziri mkuu, mawaziri , manaibu waziri na mwanasheria mkuu wa serikali, wote wanaendelea na nyadhifa zao kama kawaida

Hivyo basi, Rais aliyeko madarakani anapofariki dunia, hiyo haimfanyi makamu wake wa Rais kuwa Rais mteule,bali makamu wa Rais ataapishwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,kutokea kwenye nafasi yake ya makamu wa Rais

Mheshimiwa Rais mama Samia Hassan Suluhu, kabla ya kula kiapo chake jana, hakuwa Rais mteule, bali alikuwa ni makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, ndio maana hata baada ya kula kiapo, baraza la mawaziri liliendelea kuwepo na mara tu baada ya kiapo, alienda kuongoza kikao cha baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza kama Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania

Japo sasa, baada ya kushika madaraka ya Rais, mheshimiwa Rais mama Samia Hassan Suluhu, anaweza kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri kwa kadri atakavyoona yeye inafaa na kwa muda atakao amua yeye

Ngamanya Kitangalala Mwaswala
0756 669494
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…