Haramu kivipi?? Huko Vijijini Watanzania wanatakiwa wapelekewe systems za kuzalisha Bio Gas inayotokana na mabaki ya vyakula, Shambani n.k. Amewagawia Mitungi sawa je Ges ikiisha wana pesa ya kununua mipya?? Wakati ata elfu Tano za kuchangia watoto wao waliopo mashukeni ni shida kutokana na vipato vyao duni! Wewe mfano kule kijijini Kwenu Mama ako , Wajomba na Shangazi zao wana pesa za kununua mitungi ya Ges anayoisambaza Mweshimiwa??? Yetu macho ila yana Mwisho haya. Watanzania ipo Siku Mungu atawapigania nao watakaa kimiya
Kijijini kwetu tunatumia kuni na mkaa, ambavyo
hatuvipati bure. Kwa kuendelea kutumia kuni na mkaa tunamaliza misitu, tukimaliza misitu mvua zinapungua, mvua zikipungua wakazi wa Daslam (na kwingineko) mnatangaziwa mgao wa maji na umeme. Mnaambiwa Kidatu, Mtera na Ruvu chini kina cha maji kimepungua.
Yeyote atakayetusaidia kutupa mitungi ya gesi bure, ili sisi tujaze gesi kwa pesa zetu, atakua ametusaidia, na ameisaidia misitu.
Kama kwa sasa serikali
haitununulii mkaa na kuni, basi hakuna hoja katika
kutaka serikali itununulie gesi pale mitungi itakapoishiwa gesi.
Suala lako la bayogesi ni jambo jema sana, tena ni jema mno (kama lilivyo la gesi ya kupikia), maana yote mawili yanapunguza utegemezi katika kuni na mkaa (misitu) kwa ajili ya kupikia.
Ni vema watu wa wizara ya nishati wakatekeleza haya yote mawili kulingana na mazingira (panapofaa kuweka bayogesi pawekwe, panapofaa gesi ya mitungi pawekwe, panapofaa gesi ya mabomba pawekwe, panapofaa vyote pawekwe).
Kwa namna yoyote ile, kuendelea kutegemea kuni na mkaa kama nishati kuu ya kupikia, kutatuletea machozi mengi (na milio mingi) hapo baadae.
Nimeacha mambo mengi sana kwenye andiko lako bila kuyajadili au kuyajibu, kwa sababu nimeona sio muhimu.
Mfano: Umesema wajomba na shangazi hawawezi kumudu kujaza gesi hivyo wasipelekewe mitungi, wakati huo huo umependekeza hao hao wapelekewe biogas schemes. Maintenance costs za biogas kwangu mimi ziko juu kuliko mtungi wa gesi, halafu pia gharama za kujenga biogas kwenye kaya 10 ziko juu kuliko kugawa mitungi kwenye hizo kaya 10.