Waziri wa Madini Anthony Mavunde: Marufuku kumwingiza mgeni mwenye leseni ndogo

Waziri wa Madini Anthony Mavunde: Marufuku kumwingiza mgeni mwenye leseni ndogo

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde, amesema ni marufuku kwa mtu yeyote mwenye leseni ndogo ya uchimbaji wa madini kumwingiza mgeni au mchimbaji mwingine asiyehusika moja kwa moja na leseni hiyo.

Akizungumza Aprili 24, 2025 jijini Dodoma katika hafla ya "Kurasa 365", Mhe. Mavunde amesisitiza kuwa sheria ya madini kupitia kifungu cha 8 imefanyiwa marekebisho, ambapo sasa inabainisha wazi kuwa leseni ndogo ya uchimbaji wa madini itatolewa kwa Mtanzania pekee, na si vinginevyo.

"Hatuwezi kuendeleza sekta ya madini pasipo ushiriki kamilifu wa Watanzania. Serikali inaendelea kuwajengea uwezo wachimbaji wa ndani ili waweze kutoa mchango mkubwa kwenye sekta hii," amesema Waziri Mavunde.

Aidha, ameeleza kuwa mtu yeyote anayemiliki leseni ndogo ya uchimbaji, lakini hawezi kuchimba, hana budi kuachia nafasi hiyo kwa wale wanaoweza kufanya kazi hiyo kikamilifu.

 
Maamuzi yana manufaa na ni manzuri
lakini isiwe tu njia au janja ya kuwapokonya wachimbaji wadogo maeneo na kupeana wao kwa wao kwa kisingizio kuwa hawana uwezo
Lifanyike kwa haki
 
Back
Top Bottom