Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) leo tarehe 20 Agosti, 2023 amemuondoa katika nafasi yake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele.
Mhe. Aweso amechukua hatua hiyo kwa mamlaka aliyo nayo kupitia Sheria Namba 5 ya Usambazaji Maji Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019.