Waziri wa Maji Awesso jiuzuru upesi na DAWASA iwajibishwe

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Waziri Awesso hutoshei katika hiyo ( hii ) Wizara na muda mfupi tu uliopita nimetoka Kukusikia ukizungumza Radio One Nipashe na Kugundua kuwa hata Kichwani pia ni mtupu mno.

Unaongea ( Unatoa Maelezo ) yako Kienyeji ( Kiuswahili ) zaidi na siyo Kitaalamu na Kitaaluma halafu pia hauko that detailed na Facts zako hazieleweki vyema kwa Watu wenye Akili Kubwa kukuzidi akina GENTAMYCINE na wengine wengi hapa Jamiiforums na Kwingineko.

Pia nifikishie Salamu zangu za Uchungu kwa Watu wa Dawasa ( hasa Yule CEO Wao mwenye Tumbo Kubwa lisilo na Faida kama Tenki la Maji Goba ) kwa Kitendo cha Kutudanganya Wakazi wa Kawe ( Lugalo na Makongo Jeshini zikiwemo ) kuwa Jana Alhamisi zingepata Maji kwa Saa 24 ( kutokana na Ratiba yao ) lakini cha Kusikitisha Jana Alhamisi nzima mpaka hivi sasa naandika hivi Kawe nzima haina Maji.

Sijui Rais Samia aliona nini Kwako Waziri wa Maji Awesso mpaka akakuamini na Kukuteua kwani Mimi kama GENTAMYCINE sioni kama Unatoshea katika hiyo Wizara Muhimu na Nyeti kwa Ustawi wa Mtanzania na Mwanadamu yoyote yule hivyo nakuombea Mabaya Ili Utumbuliwe hapo hata kama Unaroga ( Unanyangindo ) sana Ili ubakie hapo.
 
Kunduchi inaenda wiki ya tatu hakuna maji,wizara ya maji inazingua
Poleni. Kuna Demu nilitaka kuja Kumtongoza na ikiwezekana hata Kumbandua huko ila kwa hii Taarifa yako nasitisha rasmi hii Nia na hili Zoezi mpaka pale nikisia Maji yamesharejeshwa huko.
 
Huyu waziri kazi yake ni kupeleka wake zake bungeni, wiki iliyopita alikuwa Misri akiomba msaada wa kuchimbiwa visima bila aibu.
 
Poleni. Kuna Demu nilitaka kuja Kumtongoza na ikiwezekana hata Kumbandua huko ila kwa hii Taarifa yako nasitisha rasmi hii Nia na hili Zoezi mpaka pale nikisia Maji yamesharejeshwa huko.
Ha ha ha ha ha
 
Poleni sana, nakumbuka shida hii, nikiwa naishi mbezi mwisho, maji yanatoka mara mbili kwa wiki, alafu unaishi nyumba ya kupanga.

Huwezi kununua Sim tank, maana litabana nafasi, inabidi uwe na ndoo nyingi sababu zinabebana, choo ya kuflash, ilikua inanilazimu kununua maji dumu 1,000 nadhani mnakumbuka pale mbezi, Stand ya zamani kuna sehemu magari ya kubebea maji yalikua yanajaa pale ili kuuza mtaani.

Maji bidhaa muhimu sana, haitakiwi kutolewa kwa mgao kabisa.
 
Waziri Awesso hutoshei katika hiyo ( hii ) Wizara na muda mfupi tu uliopita nimetoka Kukusikia ukizungumza Radio One Nipashe na Kugundua kuwa hata Kichwani pia ni mtupu mno.

Unaongea ( Unatoa Maelezo ) yako Kienyeji ( Kiuswahili ) zaidi na siyo Kitaalamu na Kitaaluma halafu pia hauko that detailed na Facts zako hazieleweki vyema kwa Watu wenye Akili Kubwa kukuzidi akina GENTAMYCINE na wengine wengi hapa Jamiiforums na Kwingineko.

Pia nifikishie Salamu zangu za Uchungu kwa Watu wa Dawasa ( hasa Yule CEO Wao mwenye Tumbo Kubwa lisilo na Faida kama Tenki la Maji Goba ) kwa Kitendo cha Kutudanganya Wakazi wa Kawe ( Lugalo na Makongo Jeshini zikiwemo ) kuwa Jana Alhamisi zingepata Maji kwa Saa 24 ( kutokana na Ratiba yao ) lakini cha Kusikitisha Jana Alhamisi nzima mpaka hivi sasa naandika hivi Kawe nzima haina Maji.

Sijui Rais Samia aliona nini Kwako Waziri wa Maji Awesso mpaka akakuamini na Kukuteua kwani Mimi kama GENTAMYCINE sioni kama Unatoshea katika hiyo Wizara Muhimu na Nyeti kwa Ustawi wa Mtanzania na Mwanadamu yoyote yule hivyo nakuombea Mabaya Ili Utumbuliwe hapo hata kama Unaroga ( Unanyangindo ) sana Ili ubakie hapo.
Du... hivi hamjui kuwa huyu ni kijana wa Mwendazake?
 
Kwanza ratiba ya maji ya nini Kwa TZ hii? Hii siyo nchi ya kuwa na shida ya maji asilani labda mvua isinyeshe Kwa miaka 50. Hapa una Ziwa Victoria, pale una Ziwa Nyasa, kule una Ziwa Rukwa, mgao wa maji wa nini?

Mkiambiwa mlipe tozo wajenge miundombinu hamtaki
 
Jinsi wanavyokabiliana na tatizo la maji🐒

images - 2022-10-28T082600.252.jpeg
 
Mgao wa maji unapo tokea maana yake mapato yanapungu, huruma inaniijia dawasa itawalipa wafanyakazi wake nini
 
Back
Top Bottom