Waziri wa Maji Juma Aweso nini sababu hasa?

Waziri wa Maji Juma Aweso nini sababu hasa?

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Jana nilikwenda ofisi ya MORUWASA - Morogoro kufuatilia maombi yangu ya kuunganishiwa maji nyumbani kwangu, niliandikiwa invoice kuwa natakiwa kulipa zaidi ya Tsh 300,000 kwa umbali usiozidi mita 8 toka lilipo bomba (wao wanaita tawi) la mamlaka hiyo ambapo wengi wamechukulia hapo.

Nikawauliza mbona bei ipo juu kiasi hicho? nikaambiwa gharama za vifaa zipo juu, nikaenda dukani mjini kuuliza bei za vifaa, nilichoshangazwa ni kwamba vifaa hivyohivyo vinauzwa kwa nusu ya bei, kwa mfano seal tape inauzwa Tsh 500 dukani, lakini wao MORUWASA wanauza Tsh 900.

Nikarudi MORUWASA na kumuuliza mfanyakazi mmoja wa Mamlaka hiyo kwanini mnatuuzia vifaa kwa bei mara mbili ya ile ya madukani, na vifaa ni vilevile na inasemekana Mamlaka inachukua kwa wauzaji haohao wa mjini si kwamba mnaagiza toka kiwandani Dsm. Mfanyakazi yule akasema ni maagizo kutoka juu, na juu ni huko Wizarani kwamo Waziri wa maji.

Swali:
  • Kwanini Waziri unatumia Mamlaka za maji kutunyonya wananchi?
  • Kwanini unaiagiza Mamlaka ya maji kutulazimisha wananchi kununua vifaa vya kuunganishia maji kwao wakati tunafahamu Mamlaka ina jukumu la kutuunganishia maji na siyo kutuuzia vifaa?
  • Sawa yawezekana kuna sababu ya msingi kufanya hivyo, lakini kwanini mnaweka middlemen wa kutuuzia vifaa kwa bei mara mbili tofauti na madukani?
  • Lengo lako ni nini kutuibia wananchi tena waziwazi?
  • Je, umetumwa na Rais kuongeza mapato kwa kutuibia?
Hii siyo sawa hata kidogo, fedha ya dhuruma haina baraka ndugu Waziri, tunaomba uwatumikie wananchi kwa haki, maagizo yako kwa hizi mamlaka kutulazimisha kununua vifaa vya maji na wakati huohuo kutupandishia bei na kutukatalia kuunganishiwa maji iwapo tutakuwa hatujanunua vifaa vyako, ni ukiukwaji wa haki zetu raia, hii inatufanya tuamini kuwa bei hizi zimewekwa ili ninyi viongozi mnufaike na makusanyo hayo, kuna tetesi kwamba huwa mnawapigia simu wakurugenzi wa mamlaka hizo kuwaomba fedha kwa mambo binafsi, sasa tunaanza kuamini kwamba mnatuhujumu wananchi ili kupata fedha haramu inayopatikana kwa dhuruma.

Nawasilisha
 
Kuna option ya kununua vifaaa vyako mwenyewe kwa kufuata specification hasa class ya mabomba, kwa nini hujafuata hizo. Ninacho jua mamlaka hailazimishi wewe kununua vitu kwao
 
Kuna option ya kununua vifaaa vyako mwenyewe kwa kufuata specification hasa class ya mabomba, kwa nini hujafuata hizo. Ninacho jua mamlaka hailazimishi wewe kununua vitu kwao
Mkuu nakuhakikishia hilo lipo nilivyoandika hapa hebu nenda pale ofisini kwao watakuambia kabisa ni lazima wakufungie vifaa vyao, kuna wenye vifaa vyao tayari wamekataliwa wanatakiwa kununua MORUWASA unless utoe rushwa
 
Back
Top Bottom