Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 62,101
- 38,487
MHESHIMIWA WAZIRI WA MAJI, HABARINI ZA UZIMA.
Pole sana na kazi zenu nyingi za kuhudumia wananchi.
Napenda kukuletea kilio cha wakazi wa maeneo ya Kawe, Mbezi Beach na Makazi Mapya, ambao kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukikabiliwa na tatizo kubwa la maji ya bomba yanayokuja na udongo mzito, hali inayotishia afya zetu.
Tumejitahidi kuwasiliana na meneja wa maji wa Kawe, lakini bado hali haijabadilika. Wamekuwa wakileta watu kuangalia tatizo, lakini hatuoni hatua za haraka wala matokeo.
Maji haya ni hatari kwa afya zetu. Watu wazima na watoto wanapata magonjwa ya fangasi na kuharisha kutokana na uchafu wa maji. Hali imekuwa mbaya kiasi kwamba watoto na hata watu wazima wanajikuna sehemu za siri hadharani, jambo ambalo ni la kusikitisha na kufedhehesha.
Kama unavyojua, hatuwezi kuendelea kuishi kwa hofu ya maji tunayoyanywa au kutumia gharama kubwa kununua dawa kila siku kwa ajili ya: Fangasi, Kuharisha, Magonjwa ya ngozi
Tunakuomba Mheshimiwa, tusaidie haraka iwezekanavyo. Maeneo haya hayawezi kupokea huduma isiyo salama, kwani afya za wananchi ni kipaumbele cha taifa. Maji ni uhai, na tunahitaji maji safi na salama kwa kila mwananchi.
Tunakuomba kwa unyenyekevu, chukua hatua. Tunateseka sana.
MUNGU AKUBARIKI NA AKUTIE NGUVU KATIKA MAJUKUMU YAKO.