Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii, naomba nitoe mtazamo wangu kuhusu Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Wenzetu wa TAWA wamekosa weledi na hawatumii kabisa taaluma zao katika kushughulikia Wanyama waliopo nje ya Hifadhi, hakika wanachofanya siyo Profesionalism na Kinahamasisha Umma wa Watanzania kuua Wanyama Ovyo Ovyo pindi wanapowaona nje ya Hifadhi.
Mwaka huu wa 2020 tumeshuhudia UPUUZI WA TAWA kule ARUSHA baada ya Tembo kuwepo eneo la Makazi akachokozwa na Bodaboda akamrarua huyo boda boda, TAWA walipoitwa walikuja wakampiga Risasi za Moto tembo na kumuuua.
Baada ya siku chache NYATI alionekana eneo la Madare Jijini Daaaslam, TAWA walipopata taarifa walikuja wakamuuua Nyati na kuondoka na Nyama zao kama kawaida yao.
Juzi tarehe 25/12
Askari wa kituo cha Mapori ya Akiba Lukwati/Piti Mkoa wa Songwe walipewa taarifa ya Simba kuonekana kwenye mapori ya Kijiji hicho walichofanya ni kuja na AK 47 za kumwaga na MaLandcruiser yao wakamuuua Simba kwa Risasi zaidi ya 15 yaaani walichakaza vibaya sana mbele ya Macho ya Wanakijiji wakabeba ule mzoga na Kuondoka nao.
Hakika Mhe.Waziri hivi vitendo havifurahishi na wala sio vya KISOMI kamweee na Havikubaliki kwenye Ulimwengu wa Kisasa. Hivi kuuwa wanyama ndio utendaji wa Kisayansi huo??? Hakuna njia nyingine ya Kistaarabu ya kuwaondoa hawa Wanyama kistaarabu kwenye maeneo wanapovamia makazi?? Hili nalo mpaka alisemee Mhe.Rais??
Au hili nalo mpaka jamii za Kimataifa za Haki za Wanyama waje watuweke kwenye ripoti zao ndio tubadilike??? Hakika Wote wanaoshuhudia Ukatili mnaowafanyia Wanyama hawafurahishwi na mnachofanya.
Badilikeni na kutumia njia nyingine za kuondoa hawa wanyama ikiwemo matumizi ya sindano za Usingizi ili kuwahamishia kwenye maeneo rasmi ili Uhifadhi uwe endelevu.
Ni mtazamo wangu tu.