Waziri wa Maliasili na Utalii, TAWA kuua wanyama kiholela haikubaliki

Waziri wa Maliasili na Utalii, TAWA kuua wanyama kiholela haikubaliki

Mkuu kwani wewe ni CEO wa TAWA mbona unawapaka mafuta sana. All in all TAWA wanapaswa kujirekebisha.
Sio CEO ila watanzia wengi ni bendera fwata upepo. Fanya utafiti wako mdogo then njoo na hoja, ningemwelewa vizuri mtoa mada angekuja na hoja ya kuuliza ili aweze kufahamishwa.

Sent from my SM-G615F using JamiiForums mobile app
 
TAWA NI JANGA KABISA.
Kwa wilaya ya Same kuna matukio ya Kiboko kuuwa watu watano ktk mto Pangani.
TAWA wameambiwa na kuja kufanya picnic tu hawajaweza chochote mara zote wanaondoka na kuwaacha wananchi wa kata za Mabilioni na Hedaru bila msaada.
Ukienda Serengeti vijiji vya Robanda kata ya Ikoma na jirani zao Simba , Chui na fisi wanakula Ng'ombe, mbuzi na ndama bila msaada.
Nachoshauri TAWA ivunjwe na majukumu ya wanyama kokote yafanywe na TANAPA.
Kiongozi naona bado pia hujaelewa kuhusu TAWA.Mimi nimefanya uchunguzi na nimebaini kuwa Tawa wanasimamia wanyama wote ambao wapo nje ya National Parks (ambazo zipo chini ya TANAPA) na Ngorongoro (NCAA).Sasa hapa umeongea maeneo ya Same (ambapo kuna ecosystem ya Mkomazi National Park) na Ikoma ni Serengeti,sasa hizi zote zipo chini ya TANAPA shida ni moja mnyama akitoka nje ya Nationa Park (TANAPA) hata kama askari wa TANAPA wapo karibu hawawezi kushughulika mpaka wasubiri askari wa TAWA ambao nao mara nyingine unakuta hayo maeneo hawana Post (Kambi).Jambo moja la kuishauri Serikali ni Kuunganisha TANAPA,NCAA na TAWA ili waache kutegeana na pia ili kuongeza tija na kupunguza gharama za uendeshaji.Shirika litakuwa moja na lenye nguvu ambalo wanawexa kuwa na Post (Kambi) almost kila wilaya inayopakana na hifadhi.
 
Subiri siku yakukute ndo utajua kama hiki unachoongea huna utaalamu nacho. Nakushauri tu, jaribu kufanya study ya assessment ya impacts za human wildlife conflicts katika vijiji vilivyopo karibu na mipaka ya hifadhi. Utakupata majibu.
Kwa hiyo solution ni kuwaua hawa wanyama pori?
 
Kwa hiyo solution ni kuwaua hawa wanyama pori?
Na kama suluhisho ndilo hilo kuna hajja gani ya kuwaita TAWA wakati wananchi pia wanauwezo wa kuwaua.
TAWA ni wasaka Kitoweo tu hawana weledi wala tija yoyote.
 
Kwanza tuwaulize TAWA, bajeti yenu ni shilingi ngapi kuweza kuwarudisha wanyama waliovamia maeneo ya watu. Maana gharama za kumlaza, kumweka kwenye gari maalumu na kumrudisha tembo au nyati mbugani zinaweza kuwa kubwa sana..
Ndio wauwe?? Nini sasa maana ya uhifadhi??period
 
Yaani Mkuu ilipaswa TAWA waanze kutuhamasisha na kutuwekea namba ya Dharura sisi Raia wa kawaida tunapowaona kwenye mazingira yetu Kenge, Chatu, Swila na Wanyama wengine adimu tuwapigie simu wakawachukue wakawahidhi lkn kwa Upuuzi wa kijinga wanaoufanya Raia nao wataona hakuna Hajja ya kuwaita ni kuuuua tu. Sijui wanatufundisha nini sisi raia wa kawaida tusio na Elimu ya Uhifadhi, inaudhi na inakera sana hapo napo utakuta Jitu limetuna Ofisini linajiiita Mkurugenzi Mkuu wakati upuuzi kama huu unaendelea kwenye Ofisi yake, shwain kabisa
Mkuu umeandika kwa uchungu mkuu. Ni kweli kuna njia bora ya kuwadhibit na sio kuua tu sbb tunaweza kuua. Wasomi ktk hii fani yapaswa wachukue nafasi zao sbb hata mimi sipendi kabisa kuua kiumbe ambacho hakina utashi lkn mwenyezi Mungu katupa Sisi binadamu akili na uwezo wa kuwadhibiti bila kuwaua. Wanyama ni mapambo, wanyama ni Urembo basi na tuwe na njia bora zaidi ya kuwahifadhi na kuwakea bila kuwadhulu au kuwaua!
 
Mkuu umeandika kwa uchungu mkuu. Ni kweli kuna njia bora ya kuwadhibit na sio kuua tu sbb tunaweza kuua. Wasomi ktk hii fani yapaswa wachukue nafasi zao sbb hata mimi sipendi kabisa kuua kiumbe ambacho hakina utashi lkn mwenyezi Mungu katupa Sisi binadamu akili na uwezo wa kuwadhibiti bila kuwaua. Wanyama ni mapambo, wanyama ni Urembo basi na tuwe na njia bora zaidi ya kuwahifadhi na kuwakea bila kuwadhulu au kuwaua!
Naona baada ya hii post hapa JF Mkurugenzi wa TAWA jana tarehe 30/12 kafanya Press na media kuweka sawa sawa hili suala. Kweli JF ina nguvu sana
 
Na kama suluhisho ndilo hilo kuna hajja gani ya kuwaita TAWA wakati wananchi pia wanauwezo wa kuwaua.
TAWA ni wasaka Kitoweo tu hawana weledi wala tija yoyote.
Hapa tunawaongelea TAWA, kwa wananchi sina tatizo nao.. Maana kwao ni ktika kujilinda... TAWA ndo wamekuwa wakizembea ktk mchakato huu
 
Ndugu
Kwanza hujui animal behaviours kwa hiyo umeandika mengi kama mwanasiasa...
Hao wanyama hawaji ktk makazi na boda boda, kwamba utaongea nao warudi.
Pili, hizo njia nyingine unazosema kama sindano inatumika pale inabidi tu.
Kwa ufupi hao wengi wanakuwa wametimuliwa ktk makundi hasa sababu ya umri. Makazi hayo mapya watarudi tu, na kama kashaonja au ona dalili za sambusa nzuri ndo kabisa.

Ktk mambo ya control sera na sheria zipo zinaruhusu.

Wapongeze badala ya kuwalaumu hao, inawezekana ndg yako au wangu, au mifugo ingeangamia.

QUOTE="mmteule, post: 37687588, member: 56194"]
Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii, naomba nitoe mtazamo wangu kuhusu Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Wenzetu wa TAWA wamekosa weledi na hawatumii kabisa taaluma zao katika kushughulikia Wanyama waliopo nje ya Hifadhi, hakika wanachofanya siyo Profesionalism na Kinahamasisha Umma wa Watanzania kuua Wanyama Ovyo Ovyo pindi wanapowaona nje ya Hifadhi.

Mwaka huu wa 2020 tumeshuhudia UPUUZI WA TAWA kule ARUSHA baada ya Tembo kuwepo eneo la Makazi akachokozwa na Bodaboda akamrarua huyo boda boda, TAWA walipoitwa walikuja wakampiga Risasi za Moto tembo na kumuuua.

Baada ya siku chache NYATI alionekana eneo la Madare Jijini Daaaslam, TAWA walipopata taarifa walikuja wakamuuua Nyati na kuondoka na Nyama zao kama kawaida yao.

Juzi tarehe 25/12
Askari wa kituo cha Mapori ya Akiba Lukwati/Piti Mkoa wa Songwe walipewa taarifa ya Simba kuonekana kwenye mapori ya Kijiji hicho walichofanya ni kuja na AK 47 za kumwaga na MaLandcruiser yao wakamuuua Simba kwa Risasi zaidi ya 15 yaaani walichakaza vibaya sana mbele ya Macho ya Wanakijiji wakabeba ule mzoga na Kuondoka nao.

Hakika Mhe.Waziri hivi vitendo havifurahishi na wala sio vya KISOMI kamweee na Havikubaliki kwenye Ulimwengu wa Kisasa. Hivi kuuwa wanyama ndio utendaji wa Kisayansi huo??? Hakuna njia nyingine ya Kistaarabu ya kuwaondoa hawa Wanyama kistaarabu kwenye maeneo wanapovamia makazi?? Hili nalo mpaka alisemee Mhe.Rais??

Au hili nalo mpaka jamii za Kimataifa za Haki za Wanyama waje watuweke kwenye ripoti zao ndio tubadilike??? Hakika Wote wanaoshuhudia Ukatili mnaowafanyia Wanyama hawafurahishwi na mnachofanya.

Badilikeni na kutumia njia nyingine za kuondoa hawa wanyama ikiwemo matumizi ya sindano za Usingizi ili kuwahamishia kwenye maeneo rasmi ili Uhifadhi uwe endelevu.
Ni mtazamo wangu tu.
[/QUOTE]

Mkuu umeongea mtoa mada ameongea mawazo yake na conclude bila kujua hili swala kiundani
Inabidi a ongeze kwenye animal behavior management
Alafu akasome mambo ya culling basically kwenye trouble animals!!
Nadhani akimaliza atajua hajui
 
Back
Top Bottom