Waziri wa Maliasili: Nani karuhusu jamii hii irekodiwe na wageni? Wanalipwa? Inatuchafua sana

Waziri wa Maliasili: Nani karuhusu jamii hii irekodiwe na wageni? Wanalipwa? Inatuchafua sana

Video za wahadzabe zipo nyingi sana mkuu.

Mtandaoni ili upate views nyingi lazima uweke kitu controversial, chenye utata aidha kichukize sana watu au kishangaze.

Travel youtubers wengi wanapenda kurecord hizo jamii za aina hiyo na sio africa tu kwa sababu hiyo.

Wapo wanaochukia, wapo wanaovutiwa, comment zote haziwezi kuwa negative.

Umesema wamaasai wanasemwa kwa mazuri nakumbuka video moja mzungu kajirekodi anakunywa nao damu kuna watu walicomment vibaya pale.

Ni marketing nzuri, hizo hasara zinapuuzika.

Hii kesi ni kama ile ya trophy hunting, tunalalamika wazungu wanaruhusiwa kuua wanyamapori lakini hatufikirii kwamba wanalipia.

Cheki hii ina 53M views, unataka kuniambia ni hasara?
View attachment 3157689

Na hao wazungu watakuwa wanalipia sidhani kama ni bure.
Haya yanayooneshwa ndiyo maisha halisi ya Wahadzabe, na picha zao huoneshwa kwenye tv za Tanzania kila mara.
 
Huu uzi ni takataka. Kaa kimya hujui lolote kuhusu utalii.
Embu twende Taratibu ...

Utalii ni kurekodi ukiwa chooni alafu useme our culture ..

Hii ID ni wewe umejitungia tu kama Chawa au ni cheo.
 
Ndugu Waziri Salam,

Kuna video za jamii ya Wahadzabe zinazoishi maisha ya kijima porini, na ni jamii "duni" kulingana na mfumo wa maisha wa kisasa...

Lakini kwa bahati mbaya sana, kuna wageni wenye asili ya Asia wamekuwa waki record mtindo wao wa maisha na ku label kama Watanzania...

Ni video zenye komenti nyingi sana za wageni, yani hadi kufika comment 20k, na wote wanaona kama hao sio watu ni wanyama..

Wakishauliza wapi, jibu ni Tanzania...

Hiyo account inaitwa Our traditional tribe... Mbaya sana, hakuna cha kujivunia ni kudhalilisha hiyo jamii, lakini zaidi kwa watu ambao hawajawahi fika Africa, wanaweza dhani watanzania tunaishi hivi....

Hata kama ni utamaduni, mbona jamii ya Kimasai inarecodiwa kwa mazuri?

Tunaweza control kipi cha ku record na kipi si cha ku record..

Mheshimiwa sana ndugu Waziri hapana, hili lipo kwenye uwezo wako...
Kama ni mbaya basi rekebisha. Hata wasiporekodiwa watakuwa tu na maisha ya kijima!! Tuache kuficha ukweli.
 
Anayecheka maisha ya Hunter Gathering ni wa kupuuza tu, Binadamu wote tumetoka huko hata huko India katika Visiwa vya Andaman na Nicobar wapo pia.

Mimi nijuavyo YOU TUBE wana Guidelines zao zinazohusu Ubaguzi nk. Wewe Mtanzania ukiona Comment ya kibaguzi au yenye lengo la kumvua Mtu utu wake palepale unaripoti.

Hakuna haja kunung'unikia Serikali au Waziri nk.

Kuna You Tuber mmoja alienda India na kusema India ni chafu alishambuliwa sana na Wahindi huko mitandaoni Imagine kusema tu India ni "chafu",, hebu fikiria kama angesema Wahindi ni Nyani??!
 
Utamaduni wa kufichaficha ,kudhibiti hata yasiyofichika sijui kwa nini tunapenda kuukumbatia
 
Ndugu Waziri Salam,

Kuna video za jamii ya Wahadzabe zinazoishi maisha ya kijima porini, na ni jamii "duni" kulingana na mfumo wa maisha wa kisasa...

Lakini kwa bahati mbaya sana, kuna wageni wenye asili ya Asia wamekuwa waki record mtindo wao wa maisha na ku label kama Watanzania...

Ni video zenye komenti nyingi sana za wageni, yani hadi kufika comment 20k, na wote wanaona kama hao sio watu ni wanyama..

Wakishauliza wapi, jibu ni Tanzania...

Hiyo account inaitwa Our traditional tribe... Mbaya sana, hakuna cha kujivunia ni kudhalilisha hiyo jamii, lakini zaidi kwa watu ambao hawajawahi fika Africa, wanaweza dhani watanzania tunaishi hivi....

Hata kama ni utamaduni, mbona jamii ya Kimasai inarecodiwa kwa mazuri?

Tunaweza control kipi cha ku record na kipi si cha ku record..

Mheshimiwa sana ndugu Waziri hapana, hili lipo kwenye uwezo wako...
kwani wanachokifanya ni uongo au ukweli?
 
Back
Top Bottom