Waziri wa Maliasili: Nani karuhusu jamii hii irekodiwe na wageni? Wanalipwa? Inatuchafua sana

Haya yanayooneshwa ndiyo maisha halisi ya Wahadzabe, na picha zao huoneshwa kwenye tv za Tanzania kila mara.
 
Huu uzi ni takataka. Kaa kimya hujui lolote kuhusu utalii.
Embu twende Taratibu ...

Utalii ni kurekodi ukiwa chooni alafu useme our culture ..

Hii ID ni wewe umejitungia tu kama Chawa au ni cheo.
 
Kama ni mbaya basi rekebisha. Hata wasiporekodiwa watakuwa tu na maisha ya kijima!! Tuache kuficha ukweli.
 
Anayecheka maisha ya Hunter Gathering ni wa kupuuza tu, Binadamu wote tumetoka huko hata huko India katika Visiwa vya Andaman na Nicobar wapo pia.

Mimi nijuavyo YOU TUBE wana Guidelines zao zinazohusu Ubaguzi nk. Wewe Mtanzania ukiona Comment ya kibaguzi au yenye lengo la kumvua Mtu utu wake palepale unaripoti.

Hakuna haja kunung'unikia Serikali au Waziri nk.

Kuna You Tuber mmoja alienda India na kusema India ni chafu alishambuliwa sana na Wahindi huko mitandaoni Imagine kusema tu India ni "chafu",, hebu fikiria kama angesema Wahindi ni Nyani??!
 
Utamaduni wa kufichaficha ,kudhibiti hata yasiyofichika sijui kwa nini tunapenda kuukumbatia
 
kwani wanachokifanya ni uongo au ukweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…