Waziri wa Mambo ya Ndani unda tume ichunguze SACCOS ya Magereza imejaa dhuluma

Waziri wa Mambo ya Ndani unda tume ichunguze SACCOS ya Magereza imejaa dhuluma

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Kwanza saccos hii imejaa watumishi wazembe na wasio na hekima katika muktadha wa huduma kwa wateja.

Askari hasa wa mikoani huwalazimu kutoa hadi rushwa ya zaidi ya milioni ili tu wasaidiwe kupata nyaraka muhimu kwa mfano zinazohusu mikopo.

Kama huna rushwa ya kuanzia laki tano na kuendelea sahau kupata huduma hasa ukiwa askari wa nje ya Dar es Salaam.

Kuna jamaa yangu leo ni mwezi wa pili unaenda hajajibiwa email yake aliyoituma ili aweze kupata mkopo benki ya Nmb kwa sababu hana pesa ya kuhonga.

Waziri Simbachawene shitukiza kwenye ofisi za hiyo saccos ili ujione lundo la nyaraka za askari wa mikoani wasiojibiwa hata kwa nyaraka ambazo ilibidi ziwe zinajibiwa ndani ya dakika 5.
 
Nilienda kuuliza bidhaa fulani hapo...duu hao wahudumu hapo ni janga.
 
Back
Top Bottom