Unataka China aiunge mkono Russia kwenye maslahi binafsi ya Russia. Unadhani mataifa huwa yanaendeshwa kienyeji hivyo? Soma hata Suez crisis ambavyo Marekani ilijikataa mbele ya Uingereza na Ufaransa, na Ufaransa ikajikataa mbele ya Uingereza mwishoni UK ikabaki yenyewe kwenye mgogoro na Egypt na hatimaye wakakubali Suez iwe mali ya Egypt.
Hakuna taifa lenye akili dunia hii linaenda kwa mkumbo. Sio kama Nyerere na matakwa yake binafsi eti Obote kapinduliwa Uganda, yeye anampa assylum hapa bongo na anakaribisha makamanda wake kupanga mashambulizi dhidi ya Iddi Amin. Tangu Otto von Bismarck awakutanishe waigawe Afrika hawakurupuki kuunga mkono lolote la rafiki yako. Ukiona wameungana ujue kuna calculations na kila mmojawapo anajua maslahi ya mwenzake. China hana maslahi na mgogoro wa Ukraine wala hafaidiki kitu. Yani akose kufanya exportation na abaniwe high end technologies kisa Russia?
Russia sio mara ya kwanza kupigana, tangu Soviet Union wamepigana Afghanistan na Mchina anawatazama, wamevunja muungano yupo, wamepigana na ugaidi ndani ya Chechnya yupo, wamepigana Georgia, wakaja kuitambua Southern Ossetia hadi annexation of Crimea kote uko Mchina yupo anawatazama. Leo hii ashiriki kwenye uvamizi wa Ukraine ili agundue nini, faida gani atapata. China ni optimistic na hawakurupuki, ile CCP wanajua madhara ya sanctions na vita kote uko wamepitia.
Uzuri China wanajua bado hawana nguvu, they are waiting for the right time. Na hawana mpango wa kuivamia Taiwan ambapo 40% ya semiconductors zote duniani ndio zinatoka. Wanavumilia co-existence waliyonayo wala Taiwan haina uwezo wa kuivamia China. Wanakaa kimachale labda Marekani ianze yenyewe ila sio wao.