- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Waziri wa mambo ya nje wa Cyprus bwana Constantinos Kombos, alitumwa kumwakilisha kamishina wa wambo ya nje katika umoja wa ulaya kuja Tanzania. Moja ya Marengo ya ziara hiyo ilikuwa ni kuangalia jinsi uchaguzi mkuu utakavyofanyika.
Ratiba ya awali ilionesha bwana Kombos angeondoka July 10. Lakini cha kustajabisha amehairisha safari Hadi July 15, Ili audhurie kesi ya Lissu.
Itakuwa mara ya kwanza Tanzania kiongozi wa umoja wa ulaya kwenda Kisutu kihudhuria kesi ya mtanzania.
Ratiba ya awali ilionesha bwana Kombos angeondoka July 10. Lakini cha kustajabisha amehairisha safari Hadi July 15, Ili audhurie kesi ya Lissu.
Itakuwa mara ya kwanza Tanzania kiongozi wa umoja wa ulaya kwenda Kisutu kihudhuria kesi ya mtanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Constantinos Kombos akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mahmoud Thabit Kombo.- Tunachokijua
- Taarifa inayosambaa Mtandaoni ikidai Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Dkt.Constantinos Kombos ameongeza muda wa kusalia nchini kutoka Julai 10, 2025 hadi Julai 15, 2025 ili ahudhurie kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti CHADEMA-Taifa, Tundu Lissu kwenye Mahakama ya Kisutu si ya Kweli
Kwa mujibu wa Taarifa rasmi ya Umoja wa Ulaya iliyotolewa kwa Umma Julai 6, 2025, ziara ya Waziri Dkt. Kombos nchini Tanzania ilipagwa kufanyika kuanzia Julai 8, 2025 na kukamilika, Julai 10, 2025.
Aidha, taarifa nyingine ya kuaminika ambayo JamiiCheck imeipata kutoka Ofisi za Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, ziara ya Dkt. Kombos imefanyika kama ilivyopangwa hapo awali hivyo hatakuwa sehemu ya watu watakaohudhuria kesi ya Lissu akiwakilisha Umoja wa Ulaya kama inavyodaiwa.
Pamoja na mambo mengine, Waziri Dkt. Kombos kwa niaba ya Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya wa Mambo ya Nje na Usalama/Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya, Kaja Kallas alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo na maafisa wengine wakuu wa Tanzania kujadili uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya, Utawala wa Kidemokrasia na ushirikiano wa kiuchumi chini ya mkakati wa Global Gateway.