Waziri wa mawasiliano kabla ya kufungia line zetu mkawafunge kwanza NIDA

Waziri wa mawasiliano kabla ya kufungia line zetu mkawafunge kwanza NIDA

D2050

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
1,919
Reaction score
1,094
Leo tarehe23_12_2019 Watanzania wengi wamejiandikisha Nida ili kupata namba za kitambulisho waweze kusajili line zao,wapo watanzania ambao hawajapata hizo namba hadi leo.wakati walishajiandikisha toka mwezi wa kumi.

waziri wa mawasiliano unapokuja hadharani kusema utazifungia line za watanzania ambao hawajasajili line zao kwa alama za vidole,huoni kuwa unawaonea,kwanini usianze na hawa NIDA? kuwafungia?

leo bado watu wanajiandikisha huko nida na watachukua mda mrefu kupata hizo namba huoni kuwa utakuwa umewaonea?ulipaswa waziri wa mawasiliano na waziri wa mambo ya ndani mkae mkubaliane kwa pamoja ili hawa nida ndio wawe wa mwanzo kuwajibika kabla ya watanzania ambao wapo wanasumbuka kila siku kwenda kufatilia namba zao huko NIDA
 
Miongoni mwa tasisi zinazoudhi ni hii mtu umejiandikisha mwezi wa 9 detail zote umeweka hadi namba ya simu umeweka cha ajabu unakaa miezi takribani miwili bila kujua kinachoendelea.

Mwisho wa siku unaamua ngoja niende ofisi za nida kufatilia namba yangu ya nida nijue tatizo ni nini kisha unaambiwa eti namba imezuiliwa kwa kua majina yamekosewa(majina ya ukoo yametofautiana) na wakati pale kwenye form uliambatanisha kiapo cha mahakama.

Kama ni kuizuia kwanini mhusika asipigiwe simu au ujumbe mfupi mapema kujulishwa mkanganyiko uliojitokeza na kipi kirekebishwe.
 
Hawa NIDA kiuhakika wanapaswa kuwajibishwa kwanza ndo wananchi wafuate. Leo kuna ndugu yangu alikuwa amejiandikisha toka oktoba na wakamwambia namba yake ataipata baada ya mwezi mmoja. Sasa cha ajabu leo tarehe 23/12/2019 ameenda kufatilia japo namba yake, ila akapigwa na butwaa baada ya kuambiwa kuwa form yake ilikuwa imeharibika. Sasa najiuliza hiyo form iliaribikia wapi wakati ilikuwa imejazwa kila kitu pamoja na mihuri husika, na alipoirejesha nida waliikagua kwanza ndipo wakampiga picha? Hawa nida hawapo makini hata kidogo na uzembe wananchi wanabebeshwa adhabu yake.
Mawaziri husika waangalie jambo hili kwa jicho LA tatu na si kukaa na kukimbilia kuwafungia wananchi mawasiliano tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie toka aug nimejiandikisha had leo bila bila
hata mimi toka mwezi wa kumi,kila nikienda namba bado ukienda tena mtandao unasumbua,mtandao unasumbua kwamaana ya mawasiliano mabovu,wanaohusika na mawasiliano waziri wao anakimbilia kwenye vyombo vya habari kutueleza watazifunga line zetu.huyu waziri nae hajielewi
 
hata mimi toka mwezi wa kumi,kila nikienda namba bado ukienda tena mtandao unasumbua,mtandao unasumbua kwamaana ya mawasiliano mabovu,wanaohusika na mawasiliano waziri wao anakimbilia kwenye vyombo vya habari kutueleza watazifunga line zetu.huyu waziri nae hajielewi


Mafuta tu hao mie sina hata presha!
 
Back
Top Bottom