Waziri wa mawasiliano kabla ya kufungia line zetu mkawafunge kwanza NIDA

Waziri alisema hawafungia nadhani hata raid alisema
 
Wananchi wanafungiwa line zao kwa makosa ya Nida,Uhamiaji na Rita haiingii akili kuwafungia wananchi wakati wanaochelewesha wanajulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We miezi miwili tu mwenzio toka mwaka jana mwezi wa nne, hata muda sina nishafuatilia nimechoka wafunge tu line zangu no way nitaishi kijima
 
We miezi miwili tu mwenzio toka mwaka jana mwezi wa nne, hata muda sina nishafuatilia nimechoka wafunge tu line zangu no way nitaishi kijima
Mi mwenyewe walinambia eti nianze mchakato upya,nishachoka kama vipi wafunge tu.
 
Kwa ninavyo mjua Jpm........line za simu hazitazimwa.... ...kumbukeni tunaelekea 2020.
 
Mi mwenyewe walinambia eti nianze mchakato upya,nishachoka kama vipi wafunge tu.
wanapoteza file za watu kisha wanakwambia anza upya kujiandikisha,hawa NIDA raisi MAGUFULI kawashindwa kuwatia adabu?
 
Nilijiandikisha mwaka jana mwezi wa pili wakati wanazunguka kijiji hadi kijiji, mtaa kwa mtaa. Wakati wanaleta picha ili kujua watakaopata vitambulisho, yangu ilikuwepo. Ajabu walipobandika namba, sikuiona ya kwangu. Ikabidi niombe taarifa zaidi mtandaoni. Jibu likawa TAARIFA HAZIPATIKANI TAFADHALI TEMBELEA OFISI ZA NIDA WILAYA YA TARIME. Niliona huu ni ujinga wa kiwango cha reli. Taarifa hazipatikani na mmejuaje niko Tarime.

Hapa nawaza moja kati ya haya
1. Warudie zoezi kwakutembea kama walivyotembea
2. Wafunge tu hii line, kwanza inadaiwa kama 160000. Tuone mimi nq hawa service providers nani atapata hasara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sijisumbui tena nasubiri wafunge laini zote, nimejisajili tangu mwaka jana hapo chuo cha mawela lakini hadi leo sijapata kitambulisho wala hiyo namba,

Yaani katika taasisi za kipumbafu Nida wanaongoza, wapumbafu sana hawa jamaa.
 
Kuna tabia ya baadhi ya watu kupuuzia jambo linapoanza, likifika mwisho kama hivi mapovu tu,
Mwingine anasema mda hana lkn mwisho ukikaribia yumo kwa fooeni tena ndefu tu hata siku 3 mfululizo sijui mda anapata wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu ndio walewale kesho wananchi wakitapeliwa kwa njia ya mtandao mnailaumu serikali, ila ikitaka kuzifungia ambazo hazijasajiliwa kwa vidole mnawalaumu tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…