Waziri wa Michezo aagiza Taifa Stars na Mwakinyo wachunguzwe

Waziri wa Michezo aagiza Taifa Stars na Mwakinyo wachunguzwe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mh Mchengerwa ameagiza BMT kuchunguza kichapo cha Taifa Stars huko Uganda , ambako walitupwa nje kabisa ya michuano ya CHAN , na pia Mwakinyo ametakiwa kuchunguzwa kutokana na kupoteza pambano lake huko Liverpool baada ya begi lake kupotea .

Chanzo : Mwananchi
 
Taifa Stars hawana organisation hawaeleweki, ile timu ipo ipo tu, hapo sioni sababu za kuchunguzana ni kupotezeana muda tu.

Mwakinyo naye ameshasema kilichomtokea, huyu waziri anatakiwa ajifunze ajue matokeo/ hali tofauti zinazomtokea mwanadamu kwenye michezo, sio kuleta huu ubabe wake usio na tija.

Asipokuwa makini atakuja kuharibu psychology za wachezaji wetu, waanze kucheza kwa hofu wakihofia wakishindwa wataenda kuchunguzwa nyumbani, matokeo yake hali izidi kuwa mbaya zaidi.
 
Serikali au yeye binafsi angeanza kuifuatilia mapema hyo Taifa Stars ningemuona wa maana. Na ishu ya Mwakinyo leo ndo wanamjua mtu from kitambo anajiinua mwenyewe si wameanza kumfatilia juzi juzi tuu hapa.
Ooow hapo sawa ulipo sema asemee kuhusu tozo hapo ndio nilikuwa sijaelewa maana yeye ni wazir wa michezo
 
Ooow hapo sawa ulipo sema asemee kuhusu tozo hapo ndio nilikuwa sijaelewa maana yeye ni wazir wa michezo
Nimesema tuu ki ujumla hata yy anaweza kututetea hizo tozo maana kuna siku watacheza wenyewe uwanjani maana watu watakosa hela za viingilio
 
Mh Mchengerwa ameagiza BMT kuchunguza kichapo cha Taifa Stars huko Uganda , ambako walitupwa nje kabisa ya michuano ya CHAN , na pia Mwakinyo ametakiwa kuchunguzwa kutokana na kupoteza pambano lake huko Liverpool baada ya begi lake kupotea .

Chanzo : Mwananchi
Wasisahau kuchunguza na tozo
 
Mh Mchengerwa ameagiza BMT kuchunguza kichapo cha Taifa Stars huko Uganda , ambako walitupwa nje kabisa ya michuano ya CHAN , na pia Mwakinyo ametakiwa kuchunguzwa kutokana na kupoteza pambano lake huko Liverpool baada ya begi lake kupotea .

Chanzo : Mwananchi
Halafu akishachunguzwa? Mwakinyo kwani mnamdai au alikuwa anawakilisha timu gani ya taifa? Kambi yake nchi ilichangia au anadaiwa bendera
 
Huyo mswahili wa Tanga wamuache tu, sidhani kama career yake itafika mbali.

Kuhusu Taifa Stars, pamoja na mambo mengine inabidi jina libadilishwe. Hatujawahi kufanya vizuri kwa jina hilo.
 
Back
Top Bottom