Waziri wa Michezo, Dr. Mwakyembe alivunja Baraza la Michezo Tanzania(BMT)

Waziri wa Michezo, Dr. Mwakyembe alivunja Baraza la Michezo Tanzania(BMT)

Bile Waziri Mkuu kusema pale bungeni angevunja kweli?
 
Yaani hili baraza halijielewi kabisa na wala haijulikani kazi yake ilikuwa ni nini hasa.
 
Bado na wale wa Riadha akina fILBERT bAYi kila mwaka wapo wao tu lakini hakuna wanachofanya pale TOC wamekalia kufanya ujanja ujanja tu
 
pic+BMT.jpg

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe

In Summary
  • Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Waziri Mwakyembe alisema baada ya agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Bungeni mjini Dodoma la kumtaka afanye mapitio na kuitathmini upya BMT ili kujiridhisha na usimamizi wake wa shughuli za michezo nchini limekuja wakati muafaka.
ADVERTISEMENT

By Imani Makongoro, Mwananchi
Dar es Salaam. Hatimaye Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametangaza rasmi kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi na wajumbe wa Baraza hilo huku akitaja kasoro kadhaa za Baraza.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Waziri Mwakyembe alisema baada ya agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Bungeni mjini Dodoma la kumtaka afanye mapitio na kuitathmini upya BMT ili kujiridhisha na usimamizi wake wa shughuli za michezo nchini limekuja wakati muafaka.

"Miongoni mwa changamoto zinazolikabili Baraza hilo na hali ya uhuria uliopitiliza katika uongozi na uendeshaji wa michezo karibu yote nchini.

"Pamoja na BMT kulalamikia uhaba wa fedha kuwa kikwazo kikubwa kinachokwamisha utendajikazi wake, Wizara ililiona zaidi hitaji la utashi, dhamira na kujituma kuliko pesa katika kutatua sehemu kubwa ya udhaifu uliotamalaki tasnia ya michezo.

"Mifano michache ni pale viongozi wa michezo kushika zaidi ya nafasi moja ya uongozi tena kwenye mchezo mmoja, ushiriki wa wanamichezo wa Tanzania nje ya nchi bila kuitaarifu BMT, mapromota wa mchezo wa ngumi nchini kuendesha shughuli zao bila kusajiliwa, chaguzi za vyama vya michezo kugubikwa na ubabe na rushwa, katiba na kanuni za vyama vya michezo kukosa uhakiki kubaini upungufu kuhusu masuala ya fedha;, tuhuma za rushwa, ubadhirifu, upendeleo, maamuzi ya kibabe ya wazi kabisa kutofuatiliwa na kufanyiwa kazi ni baadhi tu."

Waziri huyo alifafanua kwamba BMT ambayo imeundwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge Na.12 ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 1971, jukumu lake kubwa ni kuendeleza michezo, lakini kwa kipindi kirefu tasnia ya michezo imegubikwa na migogoro ya mara kwa mara ambayo imechangia sana kudumaza maendeleo ya michezo katika nchi yetu. Serikali ya Awamu ya Tano ilitarajia kwamba kupitia BMT, migogoro hiyo ingeweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

"Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha BMT, Baraza limepewa jukumu la kushughulikia masuala yote yanayohusu michezo ikiwa ni pamoja na weledi, amani, utulivu na utawala bora katika tasnia ya michezo.

Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wajumbe wote wa BMT kwa jitihada waliyofanya kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza toka wateuliwe mwaka 2015," alisema Waziri Mwakyembe huku akifafanua kwamba.

"Kwa kuzingatia kasi ya mageuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano na matarajio ya haraka waliyonayo wananchi kuiona tasnia ya michezo ikionesha tija, nimeamua kwa mamlaka niliyopewa na Sheria ya BMT na.12 ya 1967 (kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.6 ya 1971) pamoja na Kanuni zake za 1999, kusitisha uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa BMT kuanzia leo na Sekretarieti ya Baraza itaendelea kufanyakazi katika kipindi hiki," alimaliza.
Chanzo: Mwanasport
 
Asavali sasa ili na sisi tuchukue ubingwa WA Hispania na taifa stars yetu lol!
 
its like the country was not ruled in past 20 years......
 
Malinzi company kwishne!!!

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Familia ya Malinzi tafadhalini nendeni upesi pale ' Kaburini ' mkamuombe ' radhi ' yule Mama yenu wa Kambo ambaye Kaka na mdogo Mtu mlimnyanyasa hadi kumuita ' Mchawi ' wakati Yeye ndiye aliyeishi na Baba yenu Mzazi aliyekuwa ' Kipofu ' kwa miaka mingi kwani laana yake sasa si tu ' inawatafuna ' bali ' inawamaliza ' kabisa.

Ile ' dhambi ' mliyomfanyia Yule Mama yenu wa Kambo tena huku mkitumia ' Pesa ' zenu ' Kijeuri ' hakika naamini hata Mwenyezi Mungu ' amebariki ' laana ya huyo Mama Kwenu na ndiyo maana mpaka sasa ' Kaka ' Mtu kule ' Bandarini ' na ile Kampuni yake ya Clearing and Forwarding sasa ni ' hali tete ' huku ' Mdogo ' Mtu nae ' PCCB ' wameshafanya yao Kwake na ' Urais ' wa TFF ndiyo ' bai bai ' hivyo.

Poleni sana Dioniz na Jamal. Ni matumaini yangu makubwa kuwa lile ' Kaburi ' alilozikwa huyo Mama yenu wa Kambo mnalijua lilipo hivyo fanyeni ' hima ' mkatubu na mfanye ' tambiko ' Kubwa ila hakikisheni tu kuwa ' Sisi ' Watani zenu wakubwa Watu wa kutoka Mkoa wa Mara ( Musoma ) mnatushirikisha.
 
Back
Top Bottom