Waziri wa Michezo, Dr. Mwakyembe alivunja Baraza la Michezo Tanzania(BMT)

Waziri wa Michezo, Dr. Mwakyembe alivunja Baraza la Michezo Tanzania(BMT)

Tusubir watuletee kada. .

Sent from my D6503 using JamiiForums mobile app
 
Dar ameenda kufanya nn wakati .makao makuu ya wizara yako Dodoma..
 
Kama ilivyo team call me j
Hapa Tanzania kuna vijiji viwili tu (ninavyovikumbuka) vimejizoelea umaarufu wa aina yake:
1. Samunge: Kwa sababu ya Babu wa Kikombe kule Loliondo.
2. Kolomije: Kwa sababu ya Ndugu DAB.
 
Mpaka mkubwa aseme, kama alivyoongea Waziri Mkuu Bungeni ndio wameona mapungufu.

Tasnia ya filamu inapumulia mashine na bado unaambiwa kuna Baraza la sanaa, bodi ya filamu...na kuna watu wanalipwa mishahara kila mwezi.

Hivi COSOTA na Bodi ya Filamu wanafanyaje kuokoa hawa wasaniii !!?? Zaidi ya kwenda Ofisini na kunywa chai. SHAME!!
 
Hivi COSOTA na Bodi ya Filamu wanafanyaje kuokoa hawa wasaniii !!?? Zaidi ya kwenda Ofisini na kunywa chai. SHAME!!
Hawana wazo wala ushauri...tasnia ilijiinua yenyewe na inajifia yenyewe, wao role yao ni ku impose sheria tu, usifanye hivi au vile.

Sio bodi wala wizara yenye Mtu wa kukaa chini na Wasanii/wadau na kujadili tumekosea wapi tufanye nini....wao wakishajibu tu 'bajeti hakuna' wamemaliza mchezo wanasubiri mwisho wa mwezi chao kinaingia maisha yanasonga.
 
Baada ya kelele za wadau wa michezo ikiwa ni pamoja na wabunge hatimaye Waziri Mwakyembe amelivunja rasmi Baraza la Michezo Tanzania.

BMT ilikuwa chini ya uongozi wa Ndg.Dioniz Malinzi.
----
In Summary
  • Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Waziri Mwakyembe alisema baada ya agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Bungeni mjini Dodoma la kumtaka afanye mapitio na kuitathmini upya BMT ili kujiridhisha na usimamizi wake wa shughuli za michezo nchini limekuja wakati muafaka.
Dar es Salaam. Hatimaye Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametangaza rasmi kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi na wajumbe wa Baraza hilo huku akitaja kasoro kadhaa za Baraza.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Waziri Mwakyembe alisema baada ya agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Bungeni mjini Dodoma la kumtaka afanye mapitio na kuitathmini upya BMT ili kujiridhisha na usimamizi wake wa shughuli za michezo nchini limekuja wakati muafaka.

"Miongoni mwa changamoto zinazolikabili Baraza hilo na hali ya uhuria uliopitiliza katika uongozi na uendeshaji wa michezo karibu yote nchini.

"Pamoja na BMT kulalamikia uhaba wa fedha kuwa kikwazo kikubwa kinachokwamisha utendajikazi wake, Wizara ililiona zaidi hitaji la utashi, dhamira na kujituma kuliko pesa katika kutatua sehemu kubwa ya udhaifu uliotamalaki tasnia ya michezo.

"Mifano michache ni pale viongozi wa michezo kushika zaidi ya nafasi moja ya uongozi tena kwenye mchezo mmoja, ushiriki wa wanamichezo wa Tanzania nje ya nchi bila kuitaarifu BMT, mapromota wa mchezo wa ngumi nchini kuendesha shughuli zao bila kusajiliwa, chaguzi za vyama vya michezo kugubikwa na ubabe na rushwa, katiba na kanuni za vyama vya michezo kukosa uhakiki kubaini upungufu kuhusu masuala ya fedha;, tuhuma za rushwa, ubadhirifu, upendeleo, maamuzi ya kibabe ya wazi kabisa kutofuatiliwa na kufanyiwa kazi ni baadhi tu."

Waziri huyo alifafanua kwamba BMT ambayo imeundwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge Na.12 ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 1971, jukumu lake kubwa ni kuendeleza michezo, lakini kwa kipindi kirefu tasnia ya michezo imegubikwa na migogoro ya mara kwa mara ambayo imechangia sana kudumaza maendeleo ya michezo katika nchi yetu. Serikali ya Awamu ya Tano ilitarajia kwamba kupitia BMT, migogoro hiyo ingeweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

"Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha BMT, Baraza limepewa jukumu la kushughulikia masuala yote yanayohusu michezo ikiwa ni pamoja na weledi, amani, utulivu na utawala bora katika tasnia ya michezo.

Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wajumbe wote wa BMT kwa jitihada waliyofanya kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza toka wateuliwe mwaka 2015," alisema Waziri Mwakyembe huku akifafanua kwamba.

"Kwa kuzingatia kasi ya mageuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano na matarajio ya haraka waliyonayo wananchi kuiona tasnia ya michezo ikionesha tija, nimeamua kwa mamlaka niliyopewa na Sheria ya BMT na.12 ya 1967 (kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.6 ya 1971) pamoja na Kanuni zake za 1999, kusitisha uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa BMT kuanzia leo na Sekretarieti ya Baraza itaendelea kufanyakazi katika kipindi hiki," alimaliza.


Chanzo: Mwanasport

My Take:
Kiukweli hili baraza liliikuwa halieleweki na lilikuwa halina tija katika michezo.
Huku dioniz malinzi kule kwingine malinzi yule rais. Duuh, shikamoo wahaya.

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Mwakyembe nakuunga mkono 100% kwa kuvunja BMT sijaona kazi yoyote wanayofanya zaidi ya kudidimiza maendeleo ya mpira nchini.
 
Back
Top Bottom