Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,558
- 7,935
Waziri ashatu anasema watanzania mnakula mayai 119 kila mwaka unakubaliana naye au muongo huyu ? au kuna mtu anawasaidieni kula mayaiyenu hayo kati ya 119 kwa mwaka mpaka takwimu ziwe hivi ?
Alikuja akawauliza mitaani au yeye mtaani haonekani wala kwenye mifugo haonekani alafu anaongea tu na yeye aonekane ameongea ?
===
Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kutokana na kuimarika kwa biashara ya mazao ya mifugo nchini kwa Mwaka 2024/2025, kumechangia kuongezeka kwa ulaji wa mazao ya mifugo.
Bungeni Mjini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka 2025/26, Dkt. Kijaji amebainisha kuwa kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mtu mmoja kimeongezeka kutoka wastani wa lita 67.5 Mwaka 2023/2024 hadi lita 68.1 Mwaka 2024/2025, ulaji wa nyama kutoka kilo 16 Mwaka 2023/2024 hadi kilo 17.6 Mwaka 2024/2025 na ulaji wa mayai kutoka 107 Mwaka 2023/2024 hadi 119 Mwaka 2024/2025.
Aidha, Waziri Kijaji ameongeza kusema kuwa pamoja na ongezeko hilo, ulaji wa mazao hayo kwa mtu mmoja mmoja bado haujafikia viwango vinavyopendekezwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ambavyo ni lita 200 za maziwa, kilo 50 za nyama na mayai 300.