Waziri wa Nishati aridhishwa na kazi ya ujenzi wa njia ya umeme kuelekea Stiegler's Gorge

Waziri wa Nishati aridhishwa na kazi ya ujenzi wa njia ya umeme kuelekea Stiegler's Gorge

Naton Jr

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
7,867
Reaction score
19,250
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameeleza kuridhishwa kwake na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha Umeme wa msongo wa kV 33 inayojengwa kuelekea eneo litakalotumika kuzalisha Umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge).

Dkt. Kalemani aliyasema hayo mkoani Morogoro wakati alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa kazi ya maandalizi ya ujenzi wa mradi wa Stiegler’s Gorge utakaozalisha umeme wa kiasi cha megawati 2100 pamoja na kuzungumza na wananchi katika vijiji vinavyopitiwa na miundombinu hiyo ya kusafirisha Umeme.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa Umeme wa Stiegler’s yanajumuisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Barabara na usafirishaji Umeme kuelekea eneo la Mradi ili mradi huo mkubwa utekelezwe kwa ufanisi.

Alieleza kuwa, ujenzi wa miundombinu hiyo ya usafirishaji umeme unatekelezwa na kampuni ya ETDCO ambayo ni kampuni tanzu ya TANESCO na kwamba miundombinu hiyo inajengwa kutoka katika kituo cha kituo cha kupoza umeme cha Msavu hadi Mto Rufiji ambapo ni takriban kilometa 170.

“Kwa Vijiji ambavyo vinapitiwa na mradi huu wa njia ya kusafirisha umeme, wananchi watafungiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama ilivyo katika vijiji vingine vinavyopitiwa na miradi ya usambazaji umeme vijijini na hakuna fidia kwa wananchi watakaopisha miundombinu hii,” alisema Dkt Kalemani. Alisema kuwa, mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge unatarajiwa kuanza
kutekelezwa mwezi Februari mwaka huu mara baada ya Mkandarasi kupatikana na kwamba ujenzi wa miundombinu ya
usafirishaji umeme kuelekea eneo hilo la mradi umetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 80 na utakamilika mwezi Aprili mwaka huu.

Meneja Mradi wa Stiegler’s Gorge kutoka TANESCO, Florence Gwang’ombe, alisema kuwa mradi huo wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme utaboresha upatikanaji wa umeme katika maeneo ambayo hayakuwa na Umeme ikiwemo baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Morogoro, vijiji vya Matombo, Dakawa, Kisaki pamoja na kambi ya Maafisa wa Wanyamapori ya Matambwe.

Alisema kuwa, mradi unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 6.1 hadi kukamilika kwake na kwamba nguzo zinazotumika katika mradi huo ni za miti na zege na katika sehemu nyingine umeme utasafirishwa kwa kutumia nyaya zitakazopitishwa ardhini.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo alimpongeza Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya uamuzi wa kuanza kutekeleza mradi huo wa Stieglers Gorge ambao alisema kuwa utaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini, utainua
uchumi wa nchi kutokana na kuchochea uanzishwaji wa viwanda pamoja na maendeleo ya mtu mmoja mmoja kupitia shughuli mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme.
 
"hakuna fidia kwa wananchi watakaopisha miundombinu hii,” alisema Dkt Kalemani".

This is so sad.
 
"hakuna fidia kwa wananchi watakaopisha
miundombinu hii,” alisema Dkt Kalemani".

This is so sad.
Hii ni kawaida sana TZ, wananchi huachia maeneo yao willingly kupisha miradi ya maendeleo. Hasa nguzo za umeme, imekua kama desturi sasa. Ndyo maana Dr Kalemani akaongea hivyo. Ila ikitokea mwananchi akagoma serikali haina jinsi lazima walipe fidia kwa mujibu wa sheria.

Ila uzuri huku wananchi waka waida wana ardhi kubwa, kuachia viatua viwili siyo ishu, kwa Kenya itakua ishu kwasababu mtu utamwambiaje akuachie atua mbili wakati ndyo hiyo hiyo anayo.
 
Akirudi tena unitagg!
 
Hakuna fidia kwa wananchi watakaopisha miundombinu hii,” alisema Dkt Kalemani.

Hivi unamaanisha ni mimi sijamuelewa Dkt Kalemani?
 
hakuna fidia kwa wananchi watakaopisha
miundombinu hii,” alisema Dkt Kalemani.

Hivi unamaanisha ni mimi sijamuelewa Dkt Kalemani?
Sasa tatizo lako ni nini?
Umeambiwa sehemu nguzo zinapita wanaunganishia umeme.
 
Hii ni kawaida sana TZ, wananchi huachia maeneo yao willingly kupisha miradi ya maendeleo. Hasa nguzo za umeme, imekua kama desturi sasa. Ndyo maana Dr Kalemani akaongea hivyo. Ila ikitokea mwananchi akagoma serikali haina jinsi lazima walipe fidia kwa mujibu wa sheria.

Ila uzuri huku wananchi waka waida wana ardhi kubwa, kuachia viatua viwili siyo ishu, kwa Kenya itakua ishu kwasababu mtu utamwambiaje akuachie atua mbili wakati ndyo hiyo hiyo anayo.
Kwa vijijini sio tatizo sana maana unakuta mwananchi mmoja anamiliki eneo kubwa.
 
Back
Top Bottom