Aisee! Kwa hiyo ulitaka mtoto wako atumiwe nauli na serikali huko huko aliko!! Huu utaratibu uliwahi kuusikia wapi ndani ya hii Jamhuri yetu? Malipo ya serikali hayafanyiki kwa mtindo huo.
Kwanza unatakiwa kushukuru huyo mtoto wako kupata hiyo nafasi. Maana kuna maelfu ya wahitimu waliomba hizo nafasi kiduchu, na bado walikosa! Huku wakiwa na sifa za kuajiriwa.
Hivyo nakushauri kuuza mahindi, mpunga, mbuzi, sungura, mbwa, kuku, nk ili mtoto apate nauli ya kwenda kuripoti kituo chake kipya cha kazi, na pia umpe na hela ya kujikumu mpaka hapo atakapo jaza mkataba wake wa ajira na serikali, ili kupata stahiki zake.