Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Umenielewa nilichokiandika kweli!Kupata nafasi hakumfanyi apoteze haki yake, ivi hujui pesa ya kujikimu ni nini?
Ni hivi; serikali haina huo utaratibu wa kutuma nauli kwa waajiriwa wake wapya.
Kinachofanyika ni mwajiriwa mpya kuripoti kituo chake kipya cha kazi kwa kujigharamia mwenyewe nauli, na pia hela yake ya kujikimu, mpaka hapo atakapojaza mkataba na taarifa zake muhimu za kuonesha yuko kituo chake cha kazi.
Labda kama mtoa mada angesema mtoto wake ameripoti kituoni na kuanza kazi, halafu serikali imemtelekeza pasipo kumlipa mshahara wake, au posho ya kuripoti kituoni.