Tunakuomba Waziri wa TAMISEMI kushughulikia matatizo ya watumishi, hasa waajiriwa wapya katika kada ya elimu nchini. Tumekuwa tukinyanyasika kwa kutopata stahiki zetu za kiutumishi, hususan fedha za kujikimu.
Wengi wetu tuliajiriwa ndani ya siku 100 za Mama Samia mwezi Januari. Hata hivyo, Halmashauri zimekuwa hazitupi fedha hizo za kujikimu hadi leo, licha ya kwamba kwa utaratibu zinapaswa kulipwa ndani ya siku saba.