Waziri wa Ulinzi, Dkt. Stergomena akutana na wanajeshi wastaafu wa JWTZ

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amekutana na kuzungumza na Wanajeshi wastaafu kutoka Jimbo la Uchaguzi la Kawe Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuangalia namna ya kuzitatua.

Mkutano huo uliratibiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Askofu Josephat Mathias Gwajima (Mb) na kuhudhuriwa na wastaafu wa vyeo mbalimbali, waliostaafu kwa tarehe na ujuzi tofauti mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Jacks (Jacks Hall) uliopo eneo la Africana Kunduchi.

Waziri alianza kwa kumshukuru Askofu Gwajima kwa kufanikisha mkutano wake na Wastaafu kutoka jimboni kwake, pia alimshukuru Rais kwa jitihada zake za kuhakikisha watu wake wako vizuri.
Tatu.JPG

Dkt. Stergomena alibainisha wazi kuwa umuhimu wa mkutano na wastaafu hao kwani umemuwezesha kukutana, kubadilishana nao mawazo na pia kuangalia mfumo mzuri utakaowawesha wastaafu hao kutoa hoja zao kwa lengo la kutatua changamoto zao.

Aidha, Waziri wa Ulinzi na JKT aliwahakikishia wastaafu hao kuwa Wizara yake na Serikali kwa ujumla inawathamini wastaafu na inazifahamu changamoto zote zinazowakabili na tayari baadhi ya changamoto mchakato wa kuzifanyia kazi umeshaanza na kuwaahidi kuwa Wizara inazichukua changamoto zilizowasilishwa katika mkutano huo amezichukua. Aidha, Wizara kupitia Makao Makao Mkuu ya Jeshi itajitahidi kuzitatua changamoto hizo.

Kwa upande wake, Askofu Gwajima akizungumza kwenye Mkutano huo, amemshukuru Rais Samia kwa maelekezo yake yanayowataka viongozi katika maeneo yao kuwasiliza wastaafu wote katika maeneo yao.
Moja.JPG

“Namshukuru Mheshimiwa rais kwa maelekezo yake ya kututaka tuwasikiliza, kuwajali na kuwasaidia wastaafu wote katika maeneo ya Majimbo yetu,” anasema.

Mkutano ulihudhuriwa pia na Kamishna wa Maendeleo na Utafiti kutoka Wizara ya Ulinzi na JKT, Meja Jenerali Salum Othman, Mkuu wa Tawi la Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Paul Simuli, pamoja na baadhi ya Wakuu wa Matawi na Wakurugenzi kutoka Makao Makuu ya Jeshi pamoja na wastaafu.

Mbili.JPG

Chanzo: JWTZ
 
Anataka nini, au kutengeneza kikosi cha kwenda Ukraine
 
Sasa hao wastaafu wanafaida gani kwa sasa?tuna vijana wamehitimu kutoka vyuo vikuu na hawana kazi hao ndio inabidi wasaidiwe,sasa hao wazee wanafaida gani,wasaidiwe na watoto wao
 
Uzee sio ajali ndugu yangu kila mtu ana umuhimu wake
Kila mtu anaumuhimu,lakini sio kila mtu ana umuhimu Sawa kitaifa,Taifa linahitaji vijana wazalisha mali zaidi kuliko wazee walioishastaafu,hata mie nitazeeka,lakini huwezi kutumia rasilimali za nchi kuzungumza na wazee na kutafuta maslahi ya wazee harafu unawaacha vijana.wazee Wana umuhimu kwa familia zao,vijana wakiwezeshwa,nchi itakuwa poa kiuchumi na hao wazee watapata pesheni zao bila shaka,hata hao vijana ninaowazungumzia ni watoto wa Hawa wazee.ukiwezesha watoto watano wa Mzee mmoja,huyo Mzee atafsidika zaidi,lakini ukimwezesha mstaafu mmoja,anawasaidia vipi vijana wake jobless waliopo nyumbani!?
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amekutana na kuzungumza na Wanajeshi wastaafu kutoka Jimbo la Uchaguzi la Kawe Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuangalia namna ya kuzitatua.

Mkutano huo uliratibiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Askofu Josephat Mathias Gwajima (Mb) na kuhudhuriwa na wastaafu wa vyeo mbalimbali, waliostaafu kwa tarehe na ujuzi tofauti mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Jacks (Jacks Hall) uliopo eneo la Africana Kunduchi.

Waziri alianza kwa kumshukuru Askofu Gwajima kwa kufanikisha mkutano wake na Wastaafu kutoka jimboni kwake, pia alimshukuru Rais kwa jitihada zake za kuhakikisha watu wake wako vizuri.
Dkt. Stergomena alibainisha wazi kuwa umuhimu wa mkutano na wastaafu hao kwani umemuwezesha kukutana, kubadilishana nao mawazo na pia kuangalia mfumo mzuri utakaowawesha wastaafu hao kutoa hoja zao kwa lengo la kutatua changamoto zao.

Aidha, Waziri wa Ulinzi na JKT aliwahakikishia wastaafu hao kuwa Wizara yake na Serikali kwa ujumla inawathamini wastaafu na inazifahamu changamoto zote zinazowakabili na tayari baadhi ya changamoto mchakato wa kuzifanyia kazi umeshaanza na kuwaahidi kuwa Wizara inazichukua changamoto zilizowasilishwa katika mkutano huo amezichukua. Aidha, Wizara kupitia Makao Makao Mkuu ya Jeshi itajitahidi kuzitatua changamoto hizo.

Kwa upande wake, Askofu Gwajima akizungumza kwenye Mkutano huo, amemshukuru Rais Samia kwa maelekezo yake yanayowataka viongozi katika maeneo yao kuwasiliza wastaafu wote katika maeneo yao.

“Namshukuru Mheshimiwa rais kwa maelekezo yake ya kututaka tuwasikiliza, kuwajali na kuwasaidia wastaafu wote katika maeneo ya Majimbo yetu,” anasema.

Mkutano ulihudhuriwa pia na Kamishna wa Maendeleo na Utafiti kutoka Wizara ya Ulinzi na JKT, Meja Jenerali Salum Othman, Mkuu wa Tawi la Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Paul Simuli, pamoja na baadhi ya Wakuu wa Matawi na Wakurugenzi kutoka Makao Makuu ya Jeshi pamoja na wastaafu.

Chanzo: JWTZ
Taarifa zilisema hao ni wafuasi wa CCM na kikao kiliandaliwa na mbunge wao akutane na wanaccm wanajeshi wastaafu.
 
Back
Top Bottom