JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Waziri Stergomena amemtembelea Jenerali Mboma akiwa ni mwendelezo wa utaratibu wake aliojiwekea wa kuwatembelea na kufanya Mazungumzo na wastaafu hao tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan.
Stergomena alianza utaratibu huo, kwa kumtembelea Mkuu wa Majeshi wa Kwanza, Jenerali (Mstaafu) Mirisho Sami Hagai Sarakikya, akifuatiwa na Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Msuguri na Jenerali (Mstaafu) Davis Adolf Mwamnyange.
Wakuu wa Majeshi waliowahi kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) tangu kuanzishwa kwake Septemba 01, 1964 ni:
Jenerali (Mstaafu) Mirisho Sami Hagai Sarakikya (1964 - 1974)
Marehemu Jenerali Abdallah Twalipo (1974 – 1980)
Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Msuguri (1980 - 1988)
Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (1988 -1991)
Jenerali (Mstaafu) Robert Philemon Mboma (1991 - 2001)
Jenerali (Mstaafu) George Mwita Waitara (2001 - 2007)
Jenerali (Mstaafu) Davis Adolf Mwamunyange (2007 - 2017)
na Jenerali Venance Salvatory Mabeyo (2017 - sasa).