F16 Falcon
JF-Expert Member
- Dec 16, 2022
- 750
- 1,645
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Christine Lambrecht amejiuzulu kwenye nafasi, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC Swahili).
========
- Hatua ya Ujerumani kuisaidia Ukraine silaha kufuatia mapigano yanayoendelea baina ya taifa hilo na Urusi, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ameoomba kuachia nafasi hiyo kutokana na uamuzi huo.
Dar es Salaam. Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Christine Lambrecht amejiuzulu kwenye nafasi, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC Swahili).
Uamuzi wa kiongozi huyo unatokana na ukosaji mkali alioupata kutokana na uamizi wa kupeleka silaha nchini Ukraine na uwekezaji mkubwa alioufanya katika jeshi.
Katika mkesha wa Mwaka Mpya, kiongozi huyo alituma ujumbe katika ukurasa wa Instagram akizungumzia mgogoro wa Urusi na Ukraine huku mirindimo ya milipuko nyuma yake ikisikika hali ambayo ilizua utata.
Kufuatia video hiyo, hasira za kumtaka kiongozi waziri huyo ang’oke zilielezwa na uvumi wa waziri huyo wa ulinzi kujiuzulu wadhifa huo ulisambaa zaidi wiki iliyopita.
Mapema leo Jumatatu Januari 16, 2023 Lambrecht amesema, “Kwa muda mrefu vyombo vya habari vinanitazama mimi binafsi. Haviruhusu mjadala wa wazi kwa jamii kuhusu nafasi ya jeshi na sera za usalama za Ujerumani, kwa hiyo nimeamua kuachia nafasi yangu.”
========
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ajiuzulu