Waziri wa utamaduni sanaa na mchezo, Dr Harrison mwakyembe kuwakutanisha Diamond na Alikiba

Waziri wa utamaduni sanaa na mchezo, Dr Harrison mwakyembe kuwakutanisha Diamond na Alikiba

De wa sheria badala ya kwenda kupiga nondo darasani yupo mtaani anafanya kazi za kina Mange
 
Anazungumzia chochote kuhusu vyeti vya Bashite?!
 
Huyu nae asitake kunichanganya sasa wakipatana mim nijikute nasikiliza nyimbo zao wote hiyo haipo lazima bifu liendelee ili nibaki namshabikia diamond mpaka tone la mwisho
 
Nani anajua idadi ya medali tulizovuna kwenye mashindano ya mbio za nyika zilizofanyika Uganda wiki iliyopita.

Naomba niwe mkweli mwakyembe anafanana sana na Bulicheka.
 
Tatizo sie ambao sio celebrity tunadhani kwamba hao macelebrity ni tofauti na sie kumbe nao ni binadamu kama sie yaani kuwa wanamuziki haimaanishi kwamba mnatakiwa muwe karibu, tuchukulie mfano tu huku uraiani unaweza ukawa mtu wa soka lakini bado haihalalishi kuwa na rafiki mtu wa soka kisa mpo kwenye tasnia moja. Pia mwingine anaweza akawa mwalimu the same sio lazima kila ambae ni mwalimu lazima awe mshikaji wako. Mantinki hapa wanaweza wakawa si watu wa karibu kivile lakini bado wakawa hawana ugomvi ila sie wananzengo tunalazimisha wawe karibu
 
Kuna magonjwa ni hatari sana kwa ustawi wa afya ya akili.
 
Ruge aliwahi kusema akihojiwa kuwa Kama Ugomvi wao ni wa kutengeneza Pesa Jukumu letu ni kuuchochea sio kuupatanisha!

Kama ni Ugomvi usio na faida ndio usuluhishwe, sasa Mwakyembe sijui Kama analijua Hilo!

Alimaliza hapo akasuluhishe Ugomvi wa Simba na Yanga
 
Baada ya ugomvi kuisha hapo hapo na mwisho wa ali kiba
 
Waziri wa sanaa anatarajiwa kuwakutanisha kiba na diamond mjini dodoma ili kuweza kuwapatanisha na kuondoa tofauti zao, wakali hao wameteuliwa kwenye kamati ya team ya taifa serengeti boys

Je atafanikiwa kuwapatanisha ndo swali lililopo maana mpk sasa mmoja bado anaonyesha bado beef analipenda..!!!

Mwakyembe bado mgonjwa na hajui mambo ya muziki; anafikiria hiyo gimmick kuwa Diamond na Kiba ni maadui anadhania ni kweli kumbe wenzie wafanya biashara ya muziki wanaitumia kama PROMOTION ya kazi zao!!
 
Lakin akae akijua kajishalilisha ye ni mwanasheria kutoa matamko yasiyo na mashiko kisa kasema mtu
 
Huyu Waziri ni jipu aisee, anaamini kwa "kusikia" kuwa Diamond na Ali Kiba wana ugomvi lakini haamini kuwa Daudi Bashite alivamia Clouds pamoja na kwamba ameona CCTV video, shwain kabisa!
 
Mbona kuna mambo mengi ya msingi kuliko ya kiba na mond, angeshughulikia uhuru wa habari kwanza ningempa heko
 
As a first duty in offices..?
kwani hakuna mengine ya msingi zaidi kuliko hili ambalo halina maslahi ya kitaifa?
 
Back
Top Bottom